RICHIE atoka na "Diana" Kipimo cha Ndoa Bora

Monday, April 30, 2012 0 Comments


NYOTA  wa filamu katika tasnia ya filamu Single Mtambalike ‘Richie’ amesema filamu ya 'Diana' ni fundisho kwa wanaume wote wanopenda kuvamia wanawake wa nje huku wakiwa na familia zao.

Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni Richie alisema kutembea nje ya ndoa  uleta mitihani katika Ndoa na kuharibu mahusiano katika familia.

“Filamu ya 'Diana' ni kipimo cha Ndoa kwani inaonyesha jinsi matatizo ambayo yanaweza kutokea  kwa kuwa na Nyumba ndogo na kusalitiwa na kukuteketeza kwa njia ya ushirikina, ukiangalia filamu hii utaona mimi nilivyopoteza kazi na mke wangu kurongwa ," alisema Richie


Amesema ujio wa filamu hiyo utatoa fundisho katika hali za kifamilia ni 'Diana' ni kipimo cha Ndoa bora.

0 comments:

Musician Recaptures Tanzanians Lost Glory

Friday, April 27, 2012 1 Comments



Tanzania has regained its lost glory in world of music fame that has dwindled since the eighties.

When the name of Tanzania is currently mentioned in international music circles the name of Ebrahim Makunja popularly known as Ras Makunja of FFU and his “The Ngoma Africa Band” aka FFU based in Germany cannot be slighted. FFU has earnestly strived to place Tanzania in the international music charts.
It is the only Tanzanian band that is based overseas. Its contribution in the music industry both in Tanzania, East Africa and abroad is superb. The band has often been able to bring its records to radio stations back at home.
Many of their hits touch the souls of their fans. Two of their hits, which are very popular in local radio stations and contained in “50 Uhuru Anniversary” CD are “Shangwe”, and “Miaka 50 ya Uhuru”. The rumba style songs are composed by band leader Ras Makunja.

1 comments:

FATMA 'MCHARUKO' wa JAHAZI kurudi tena Stejini baada ya matibabu!

Thursday, April 26, 2012 1 Comments

Fatma 'Mcharuko' akipagawisha mashabiki wa Taarab

 Mwimbaji Chipukizi wa Jahazi Mordern Taarab anayefanya vizuri ktk muziki wa Taarab Fatma Mahmoud 'Mcharuko' anatarajiwa kurudi jukwaani tena na kuwapa ile burudani wadau wameikosa kwa muda mrefu takribani mwezi sasa baada ya kupumzishwa kutokana na matatizo ya kuanguka anguka mara kwa mara


Mama wa Mcharuko alirudishwa kwao Zanzibar kwa matibabu tangu tarehe 23 mwezi March na kwa mujibu wa Mkurugenzi Fatma anaendelea vizuri sasa na hivi karibuni anatarajiwa kurudi kundini kuliendeleza libeneke.....

Fatma Kassim akak 'Mcharuko' kwa sasa anatamba sana na kibao chake cha "Mtaniona hivi hivi" na awali aliimba kile cha "Mfa Maji"

Wadau tumuombee apone haraka!

1 comments:

Happy MUUNGANO DAY...!

Thursday, April 26, 2012 0 Comments

Mwl. Nyerere na Karume wakipungia watanzania siku kama ya leo miaka 48 iliyopita ambapo waliunganisha Tanganyika na Zanzibar na kuwa TANZANIA

Leo Taifa letu linaadhimisha miaka 48 ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika, sherehe na shamrashamra za kutosha ktk uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

"Shiriki kikamilifu ktk Sensa na mchakato wa mabadiliko ktk Katiba"

NAIPENDA TANZANIA, NAJIVUNIA AFRIKA!!!!!!

KIAFRIKA ZAIDI

PROUDLY AFRICAN

0 comments:

Queen Darleen - Hakuna upendeleo Tuzo za Kili!

Thursday, April 26, 2012 0 Comments

Kwa kupata tuzo hii nimeondoa dhana kwamba wasanii waliokuwa
wanashinda walikuwa wanapendelewa,”hiyo ni kauli ya Queen Darleen
ambaye alitwaa tuzo ya wimbo bora wa Ragga/Dancehall katika tuzo za
Kili mwaka 2012.
 
“Nimefurahi sana kutwaa tuzo hizi ambazo ni kielelezo
cha ubora wa kazi za msanii husika, nawashukuru mashabiki walionipigia
kura, lakini napenda kusema kuwa tusipende kukariri hakuna upendeleo
wowote,”anasema.
 
Katika mahojiano yetu msanii huyu anasema zamani alikuwa akiamini maneno ya watu kuwa tuzo hizo zinatolewa kwa upendeleo na hivyo kumfanya kutokuwa na imani nazo kabisa.

Hata hivyo baada ya usiku huo kufanikiwa kutwaa tuzo hizo ameamua
kuachana na dhana hiyo mgando ambayo imejengeka vichwani mwa watu
wengi, hivyo kuwataka kuamini kuwa tuzo hizo anapata mtu anayestahili.
 
Darleen ambaye wimbo wake 'Maneno Maneno' aliomshirikisha Dully Sykes ndiyo umemuwezesha kutwaa tuzo hiyo akizipiku nyimbo za Good Look wa Ay ft Ms Trinity, Ganjaman wa Dabo, Kudadadeki na Poyoyo za Malfred.

0 comments:

CHEZEA CHELSEA WEWE!!!!

Wednesday, April 25, 2012 1 Comments


RAMIRES

TORREEEEEEEEEES


Chelsea 3- 2 Barca, haya waleteni hao wengine! sijui Madrid sijui Bayern

1 comments:

Chipukizi wa3 wapatikana kupiga Show na Washindi wa Tuzo za Kili Dodoma!

Tuesday, April 24, 2012 0 Comments

Majaji Kazini, hapa wakisikiliza muongozo kutoka kwa muendesha zoezi, Irene Kiwia, ambaye hayupo pichani, kutoka kushoto ni henry Mdimu, Joseph Haule, Queen Darleen, na Juma Nature

Top 20
Tatu bora, kutoka kushoto ni Halima Ramadhani, katikati ni Juma Madaraka na mwisho kabisa ni Issa Dubat       




Majaji walitumia siku 2 kuwafanyia usaili wasanii chipukizi 247 waliojitokeza kuwania nafasi 3 za kupanda jukwaa moja na washindi wa Kili Music Awards 2012 wanaotarajia kufanya show wikiendi hii ktk Club ya 84 DODOMA. 

Akitangaza washindi, mmoja kati ya majaji walioonekana kuwa chachu ya mchuano huo henry Mdimu, aliwataja Halima Ramadhani, Juma madaraka na Issa Dulat kuwa ndio waliofanikiwa kufikia vigezo vya kuwa wasanii bora kabisa kutoka mkoani Dodoma kwa mwaka huu ingawa dhahiri vipaji vilionekana kuwa vingi kuliko walivyotegemea.

"Haikuwa kazi rahisi, ilikuwa inatupa wakati mgumu na kama sio maelekezo ya waandaaji huenda tungejikuta tu8nachukua hata watano baada ya watatu", alisema Jaji huyo baada ya shughuli kuisha.

Wiki hii mpambano utaendelea katika mkoa wa mwanza, ambapo Jumamosi, wasanii wa mkoa wa Mwanza watakuwa wakiisaka nafasi hiyo katika ukumbi wa Villa Park.

0 comments:

Ndovu Special Malt yashinda tena Tuzo ya Ubora!

Tuesday, April 24, 2012 0 Comments

Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt Pamela Kikuli akiongea na wana-habari leo

Bia ya Ndovu Special Malt inayotengenezwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), imedhihirisha ubora wake kimataifa baada ya kushinda kwa mara nyingine tena tuzo ya dhahabu yenye hadhi ya juu zaidi ya ubora wa bidhaa kimataifa ijulikanayo kama “Grand Gold Quality Award”
 
Akizungumza na waandishi wa habari, meneja wa Bia ya Ndovu Bi. Pamela Kikuli alisema; Tunayo furaha kubwa sana kuwajulisha wadau wa Bia hii ya Ndovu Special Malt juu ya ushindi huu mkubwa ambao Bia hii imenyakua katika tuzo za bidhaa za kimataifa zinazotolewa na Taasisi ya kimataifa inayoangalia ubora wa bidhaa ya “Monde Selection International Quality Institute” iliyopo Brussels, Ubelgiji (Belgium). Tuzo hii yenye hadhi ya juu kabisa katika ubora wa bidhaa kimataifa inajulikana kama “Grand Gold Quality Award” na hushindanisha bidhaa toka Mataifa mbalimbali ambapo mwezi huu Aprili taasisi hiyo imetangaza rasmi kuwa “Ndovu Special Malt” imeshinda tena tuzo ya “Grand Gold” kwa mwaka 2012. Alisema Pamela.

0 comments:

MISS UTALII TANZANIA KUTANGAZA UTALII MAREKANI

Monday, April 23, 2012 0 Comments

 
Warembo wawili wa Miss Utalii Tanzania 2011, watawakilisha Tanzania katika Shindano la Dunia la Miss United Nation 2012, litakalo fanyika July 28 huko calfonia Marekani.Shindano hilo linashirikisha zaidi ya nchi 100 duniani kote.

Hii itakuwa ni fulsa nyingine ya pekee kwa nchi yetu kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania , huko nchini marekani na duniani kwa ujumla. Warembo hawa pamoja na kwenda kutangaza utalii na utamaduni wa Tanzania kwa ujumla, lakini watapeleka ujumbe mahususi kwa wamarekani na Dunia kwa ujumla juu ya mlima kilimanajaro,Seremgeti na Ngorongoro Crater kuwa viko tanzania na ni mali ya tanzania. Hii itasaidia kuondoa na kupambana na propaganda za nchi nyingine kuwa vivutio hivyo vipo kwao.

0 comments:

Kitabu cha Werrason

Monday, April 23, 2012 1 Comments

Werrason ni mmoja wa wanamuziki wa Congo wenye washabiki wengi sana hapa nchini na Africa  na Duniani  Lakini kwa muda mrefu mashabiki na wapenzi wake hao wamekua wakimfahamu Le Roi De La Forret Papaa na Exocee Mobali ya Mama Pastor Sylvie Mampata kijuu juu tu. Lakini
safari hii mashabiki wake na wa muziki kiujumla hususan wanafamilia wa
wenge wamepewa fursa maalum ya kumjua nguli huyu wa muziki wa congo
kupitia kitabu mahalamu ambacho kimeshachapishwa kikielezea historia ya mwanamuziki huyo binafsi na katika harakati zake za kujiingiza kwenye muziki, kuwa star na mpaka sasa kumiliki bendi kubwa na yenye
mafanikio makubwa .

Dondoo za yaliyomo kwenye kitabu hicho ni kwamba ndani ya kitabu hicho
werrason anaelezea kwa mfano wenge musica ilivyozaliwa. Katika hilo
Werrason anasema mwanzoni kabisa walikua yeye Werra, Aime Buanga, Jean Belix Luvutula, Didier Masela na Christian Zitu, ambapo Aime Buanga
alichukuliwa kama muanzilishi wa kundi kutoka na yeye kujitolea nyumba
ya wazazi wake alimokua akiishi itumike kama sehemu ya kufanyia
mazoezi ya kundi lao hilo na pia Didier Masela nae kwa upande mwingine
akichuliwa kama muanzilishi pia kutokana na kwamba wazo la kuanzisha
bendi lilitoka kwake

1 comments:

ISHA - 'NYIMBO ZA MAPENZI ZINACHOSHA"

Monday, April 23, 2012 1 Comments

Nyimbo za mapenzi zinachosha.

 Kama ni mapenzi yalianza tangu enzi za
Adamu na Hawa na hadi leo watu wanazungumzia mapenzi. Lakini kuna vitu
hata vikikaa miaka hamsini, ujumbe wake haufi

Na hata mie leo ningejiimbia tu  ili mradi ujumbe ufike kuna vipande vingi dida mie ninavyo kama

1:Aso komwe ana chogo,usione ukubwa wa andazi katikati kweupe,unanini uso wa baraza,wowo lako la kichina,kasugue kisigino bibi usituchanie mashuka haya sasa wale waimbaji nimewapa kidogo ila ninavingi.

 

1 comments:

ETI SERENGETI BOY,TWIGA STARS WAKO WAPIIIIIIIIII?

Friday, April 20, 2012 2 Comments

Inaitwa umbile si hoja hoja virutubisho,eti mnaosema wake serengeti boy kwani mnataka nini,kijana yuko makini haitaji msaada wa kocha Maximo yuko chini na wala haitaji msaada wa jezi kiwanda anachondani kinafyatua  vifaa kama yuko marekaniiiiiiiiii,Ilo nalo neno babu mdogo kwa wazazi wake lkn kwa hapa mkubwa mwenzie na kama mtoto mdogo mbona akienda chooni aachi mlango wazi?Na mna kadi yake ya Clinic?Nyie mnaowasema wanaume wa wenzenu wadogo mara wakubwa kwani wanabebwa mgongoni?kila mtu na mtueeeee ilo lako litakae mgusaaaaaaaaaaa.

2 comments:

MZEE YUSUF AWAPONGEZA KHADIJA KOPA NA ISHA MASHAUZI KUPATA TUZO, ..........!

Tuesday, April 17, 2012 0 Comments

Managing Director wa JAHAZI Mordern Taarab Mzee Yusuph amewapongeza wasanii wenzake wa Taarab Isha Mashauzi na Khadija Kopa kwa kupata Tuzo za muziki za Kili ktk sherehe iliyofanyika Jumamosi iliyopita Mlimani City jijini Dar es salaam

Amesema, haijamuuumiza kukosa Tuzo hizo mwaka huu, ni jambo la kawaida kwake na kwamba yeye ataendelea kuwa nambari moja ktk muziki huu wa Taarab Tanzania.

 

0 comments:

Filamu ya "Double J" kuingizwa sokoni

Tuesday, April 17, 2012 0 Comments

 

MSANII kwenye tasnia ya filamu nchini Jimmy Mponda 'Jimmy Master'amesema yuko mbioni kuingiza sokoni ujio wa filamu yake mpya iitwayo 'Double J'.

Mbali na ujio huo wa sasa , 'Jimmy Master'ambae  alishawai kutikisa na filamu ya 'Misuko Suko' ambayo ilitoka kuanzia Party 0ne hadi Party three.

Akizunguza jijini Dar es Salaam'Jimmy Master' alisema kuwa ujio huu wa hivi sasa wa filamu hiyo huko chini ya Kampuni yake iitwayo Jimpo Wood Company LTD .

"Huu ni ujio wangu mpya kwa sasa baada ya kujipatia mashabiki kwenye filamu za 'Misuko Suko' Party one hadi three,"alisema 'Jimmy Master'.

Awali 'Jimmy Master' alianza kujipatia mashabiki wa filamu kupitia filamu kama 'WOSIA' ambayo pia alifanikiwa kuibua vipaji vya wasanii wa Bongofleva. Ambapo wasanii kama Abubakari Katwira Q- Chilla pamoja na Daz Edd Waliibuliwa

0 comments: