MY WEDDING DAY....
Namshukuru sana Mungu kwa tukio hili na ninaipenda sana ndoa yangu. Mlio-post picha za simu nyingi hazikutoka vizuri, haya sasa mzigo huu hapa..... INSHAALAH!!!! Rasmi sasa Dida wa Ezden
Bi Hindu akiongea maneno yake ya msingi kwa maharusi.... Bwana mdogo hapo chini ni Deen The Next Big Thing (The Next Rocker)
Baba mzazi wa Ezden upande wake na Upande wa Dida ni uncle wa bi harusi...
Maharusi na brother wa Bi Harusi Mr. Athumani...
Kabla ya ndoa stori zilikuepo za hapa na pale....
Ndoa maalum ya KIISLAM hapo kikisainiwa cheti cha ndoa....
Ndoa maalum ya KIISLAM hapo kikisainiwa cheti cha ndoa....
A close-up shot of a wedding certificate...
Deen The Next Big Thing talking to dad, next to mum...
Cousin Brother wa Bwana Harusi Mr. Taiz, Ezden The Rocker, Dida wa E na Baba wa Bwana Harusi Mr. J4...
Deen shaking the hand of a Bi Harusi...
Dua sasa hapa...All the BLESSINGS.... Alhamdulillah...
Hii sasa ndio ndoa inafungwa aliyeshikana mkono na Bwana Harusi ni kaka wa Bi Harusi Mr. Hussein Shaibu
Kwa walio wahi kuhudhuria harusi za kiislamu kuna hii kitu wengine huita Kombe wengine huita kula solo... hapa bwana Harusi akiweka chakula ambacho anaenda kula mkewe, kama hujui kuhusu hii kitu uliza kwa waislamu wakupe zaidi. Misosi kibao, mwendo wa draft hapo dah....!!!!!
Mdogo wa Bwana Harusi Sufian Jumanne na upande wa Bi harusi ni mashost.... pamoja sana!!!
It is what it is.....!!!!
Maharusi na Mama Ezden (Mama mzazi wa Bw. Harusi...
Mama Ezden (Bi Saada) akimpatia mkwe wake zawadi ya Khanga....
Toka Times Fm 100.5 anaitwa Mariam Kitosi wa Hatua Tatu program akiwa amepozi na maharusi...
Hii sector achana nayo kabisa ndugu yangu....
Mamaa Dotnata naye alikuwepo kutupa support, shukrani sana mama etu....
Mama na wanae...
Mama mzazi wa Dida hapo kati akifurahi siku hii muhimu.... Asante mama, tunakupenda sana....
Bi Hindu, Ezden, Deen, Mama Ezden, Dida na Mama Dida...
No caption ndugu zangu....
Kutoka Times Fm 100.5 ni waiziri wa WIZARA ya Michezo Mr. Clifford Mario Ndimbo akiweka pozi swafi na maharusi... Thanx a lot brother kwa support
VJ Penny, Ezden, Deen, Dida na Sauda Mwilima... Thanx our friends...
Mamaa Sandrah, thanx alot kwa support...
Matron Sauda Mwilima pamoja sana ndugu....
Dua sasa ya bwana harusi anyomwombea mkewe baada ya kupewa mke....
Ustaadh aliyefungisha ndo hii Sheikh Mtiga....
Hapa katika picha ya pamoja na wazazi wetu...
Wazazi.... Tunashukuru sna kwa yote mazuri....
Na baada ya ndoa ni ndani ya Range na kuelekea kunakohusika. Usikose kufuatilia kilichoendelea hapa hapa baadae kidogo..... Tunawashukuru wote walio na sisi wakati wote, na wale wenye chuki tunawapenda pia...!!! IME-HAPPEN
hongera na kaza moyo dida mumeo bado mdogo sana kwako, yasiwe kama yaleeeeee ya kutazama cm yake.na vj penny anaangalia ndoa za kiislam anajipa hope na yeye ataolewa, ndoa msifikiri lele mama kama mashauzi ya kujionyesha kwenye kompyuta lol
ReplyDeleteMabrouk inshaallah allah awape masikilizano Ameen
ReplyDeleteDida sema ukweli wako jinsi ulivyosikia raha ck ya hii ndoa ya KIISLAAM..kuliko ile nyingine ya serekali!SEMA HUJAJISIKIA KM MISS WORLD HII KITU YA KIISLAAM ACHANA NAYO MOLA NDIYO ANAJUA NINI NDANI YAKE.. Nimefurahi sana sana and I wish u all the best..RAMADHAN KAREEM.
ReplyDeleteAllah akusimamie kwenye ndoa yk!
ReplyDeletehongera sana Dida, umependeza sana, nakutakia kila la kheri kwenye ndoa yako
ReplyDeletendoa ya kupka futari kwikwiwiwiw
ReplyDeletealiyekwambia futari tu ndio inaliwa kwenye mkeka nani?
DeleteUtabakia hivyo hivyo ndoa ya futari wakati mwenzio yuko kwa mumewe wewe watanga na njia.
Deletenyie ndio wachawi wa maendeleo ya watu msiowapendezea wenzeo mazuri mtu anaingia kwenye mambo ya kheri mnaanza kumtabiria uchafu wenu wee mbona hata ndoa ya futari huna kauze taa taka yako mango pale shwain ewe
DeleteHongera Dida Mungu awatangulie
ReplyDeleteDuh Ezden huyu kumuoa dida .............Inshaallah na mola awajalie ila namuonea huruma bwana harusi sema nayeye anapenda sana kulelelwa hapo kafurahi sana
ReplyDeleteBi harusi kaolewa mara ya Tatu bwana harusi kaoa mara ya Pili kama wanashindana vile....mbona mwanaye Bi harusi atujamwona eeeh
huwezi jua jinsi nilivyofurahi dada kupata mume wa dini yako . nakutakia kila la kheri kwenye ndoa yako mwenyezi mungu akusimamie inshaallah muishi miaka mia nane. ukaze uzi sasa. mashaallah mumeo handsome. hongera sana sana. Dida wa E. PENDA SANA MIMI
ReplyDeletehongera,. ila hii iwe ya mwisho
ReplyDeleteWOW ! WOW! WOW! HONGER DIDAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
ReplyDeleteMWANAMKE NDOA INAHUSU KULALA NA NYEGE ??????
NASHANGAA WANAOSEMA MWANAUME MDOGO JAMANI EHEEEE SIJAONA UDOGO WA HUYO MWANAUME ACHENI MBWEMBWE
ReplyDeletemmmh we kibokooooooooo
ReplyDeleteDIDA WEWE MWANAMKE WA SHOKAA HEHEYAAAA
ReplyDeleteJL TZ HAKUALIKWA ?????
ReplyDeleteHUYO MTOTO NI WA EZDEN?
ReplyDeletebarikiwa sana Dida na mumeo. usijali waja wanasema nini. Hongereni
ReplyDeleteUsiseme yote mengine bakiza.muombe Mola wako wanaume wote baba mmoja mama mmoja.hao wote Waliokuoa mwanzo uliwapenda pia aijalishi dini gani.cha Msingi ni kumuomba Mungu sn.nipó kwenye ndoa najua ugumu wake.Mungu akusaidie
ReplyDeleteNaona vijembe na mashairi ya mipasho leo hakuna,bwana ezden nahisi ndio aliepost hapa na maneno kaandika yeye,hope na wewe dida utabadilika,acha uswahili.. Kila la kheri inshallah
ReplyDeleteSheikh Mtiga wa Mwananyamala/k'ndoni,ndo alofungisha ndoa yangu.Asante sheikh kwa kutufanikishia ndoa zetu,Mwenyezi Mungu akujaalie kher.
ReplyDeleteHongera sana maharusi,ndoa ni jambo la kher.Better kuoana kuliko kufanya zinaa.Jazaqa-allah!
ReplyDeleteKila la kheriiii mke ujiii
ReplyDeleteAsalaam alykum Bi Khadija Shaibu, mimi nataka nikuusie machache tu mdogo wangu, mengi utakuwa umeshapewa na umeshajifunza kutoka katika ndoa zilizopita. Nitaweka mtiririko wangu kwa namba.
ReplyDelete1. Jambo la kwanza na kubwa kuliko yote ni wazazi wa mumeo, Dida uende kuwa kiungio kikubwa kati ya mumeo na wazazi wake na hata nduguze wengine. Hakuna kama wazazi duniani, kama vile ambavyo wewe hutataka mtu amtendee mzazi wako mabaya, basi na mumeo hali kadhalika, watendee yale ambayo ungewatendea wazazi wako waliokuzaa. Wanaume huwa wasahaulifu sana inabidi kila mara umkumbushe mumeo kuhusu kuwatendea mema wazazi wake kwa sababu pepo yake iko chini ya miguu ya mama yake, na wewe pepo yako iko chini ya miguu ya mumeo. Sasa mumeo akikosa radhi ya mama yake ina maana na pepo yake kaikosa na wewe huna pepo hapo. Wazazi ndio alpha na omega.
Na bwana harusi pia ukumbuke mkeo ana jukumu kwa mzazi wake kama ambavyo wewe una jukumu kwa wazazi wako. Mkishirikiana katika kuwatendea mema wazazi wenu, maisha yenu yatakuwa yana baraka tele, na hata mkikorofishana wazazi wenu watakuwa mstari wa mbele kuwarudisha kwenye makubaliano.
2. Japo la pili bi kharusi na bwana harusi ni ibada, fanyeni ibada wadogo zangu dunia hii imeashavaaa bukta ni ibada peke yake ndio itakayodumisha mapenzi baina yenu. Tena muwe mnafanya ibada pamoja kwani hakuna kinga kubwa kama sala. Na hizo sala zitawakinga na mabaya ya watu na pia itawakinga na vishawishi na vitimbi vya sheitwani.
3. japo la tatu, ni madikodiko, najua unakuwa kazini muda mrefu lakini jitahidi uwe unampikia mumeo, jifunze mapishi tofauti kupitia kwenye mitandao kama alhidaya, siku hauko kazini unamsumprise mumeo na mapishi ya aina tofauti, ugonjwa wa wanaume wengi ni madikodiko. Na mume nawe wanaume wa kiislamu wanawatakiwa kuwasaidia wake zao shughuli za nyumbani hayo hudumisha pendo, akiwa anapika wewe msaidie kukatakata nyanya lol!
Mengine ushaambiwa sana ni kuyafanyia kazi, kikubwa ni kuwa hakuna aliyemkamilifu duniani, wewe una mapungufu yako na yeye ana mapungufu yake, kwa hiyo ikifika mahala ukaona kuwa huyu bwana ana mapungufu basi yatazame mapungufu yako kwanza kisha yatazame mazuri yake pia. Hakuna aliyemkamilifu, nawatakia ndoa njema iliyojaa baraka tele, mzae watoto walio wema.
Kwa wanaosema Dida mkubwa ana ukubwa gani huyu Dida?, au kwa kuwa aliolewa ndoa ya kwanza akiwa binti mdogo? Huyu Dida hana ukubwa wowote ni yeye tu mwenyewe anavyojiachia, ni mtoto mdogo sana, anakua pale Ubungo maghorofani jirani kwa mama wawili tunamuona, sie tushaolewa yeye bado mtoto mdogo. Afanye mazoezi apunguze uzito atazidi kuonekana mdogo.
Annoy hapo juu! Kwanza hongera kwa hotuba hapo juu ndeeeeeeefuuu mpk uvivu kuisomaa! Huo umri unaousema unamaanisha nn kusema mtoto mdogo! Mtu akishafikisha 30s sio mdogo tena huyo!
DeleteSasa hata kama ni hotuba hukuandikiwa wewe, aliyeandikiwa ni Dida, wewe ruka koment songa mbele.
DeleteNa aliyekwambia miaka 30 ni mkubwa nani? Mbona bado anafit umoja wa vijana huyo lol! Sasa sie wa miaka 40 tujiiteje kama wa miaka 30 wanajiona wakubwa? Mie nina miaka 42 na ndio kwanza nimeolewa na nina mimba ya mtoto wangu wa kwanza, poa kabisa.
heeee mda hongera kwa hiyo mimba jamai kumbe namimi nitajapata mimba maana ,nimeolewa nina miaka 41 sasa niko huku ulaya wanasema kuzaa itachukua muda sababu ya umri jamani nikawambia mbona dadangu kazaa na umr mkubwa 44ilinipa wasiwasi ila naona watu wengine wansema kama wwe hapa umepatamimba na 42 napata farja namimi kuwa munu atanipa mtoto,mnimbee wanawake wenzagu,dida mmependeza mumeo mzuri na wewe mmendaa sana be blesed
DeleteHongera Sana vaa buti miba isipate nafasi
ReplyDeleteHongera wajina usiskize ya watu! Kinachotakiwa mpende mumeo naye atakupenda inshaallah
ReplyDeletehongera dida ndugu yangu mwenyezi mungu aisimamie ndoa yenu wanga wasipate chance, nakuona shangazi langu wa ukweeee aunt Mariamu (mama Dida) love u mingi my aunt...
ReplyDeleteWanga utawajua tu. Sasa umri wa mtu unahusu nini kwenye mapenzi ya watu? Dida na Ezden langu moja tu ni Usiri. Yani wekeni mbali camera. Sasa nyie mmeshakuwa chanzo cha udaku. Nadhani mnajua hili. Hebu kuweni makini saaana msi expose maisha yenu. Mbona Gea Habibu kaweza? Blog fanyia biashara ingine si habari ya ndoa yako, that is kama unaipenda iyo ndoa. Mana blog zenu mashosty mnatukanana na kuumbuana hadi mie hujiuliza hizo PHD za matusi mmesoma wapi? Hongereni saaana
ReplyDeletenimependa nguo zenu,mmependeza cna,yaaani mmetokelezeaaaaaa
ReplyDeleteumependeza sana da didah achana na waswahili hawaishiwi na lakusema
ReplyDelete