MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.... KHERI KWA KILA MTU

Saturday, July 13, 2013 36 Comments

Kila la kheri katika mwezi mtukufu wa ramadhani... inshaalah Mungu atujalie kheri....!!!


Shukrani sana Mungu kwa yote mema na afya unayonijalia nami nimo katika mfungo wa ramadhani tukufu.... 

Na mume wangu Ezden, wote ndani ya mfungo...



36 comments:

  1. Mashaallah allah awadumishe dida wapendeza na dira na baibui.mdau kutoka Belgium

    ReplyDelete
  2. Umependeza mungu awabariki muishi milele ili wavimba macho wataayuri

    ReplyDelete
  3. Nimekupendaje! Mungawajaalie mzikane na ckutengana

    ReplyDelete
  4. mungu awajaalie awape baraka telee,nimefurahi sanaa kusikia umeolewa na muislam mwenzio kuliko yule mgalatia alikuwa anakutia dhambi tuu kwenye mwezi kama huu,anyway your husband is super HOT na mnapendezana wenyewee wote waremboo kwa sana tuu..

    ReplyDelete
    Replies
    1. dhambi kivipi? waosha vinywa mnaongea hadi mapovu yanawatoka na hadi mtakufuru..ukiwatakia heri na kufunga domo lako utapungukiwa nini? nyinyi ndo mtakaokuwa kuni huko kama kuna moto...shenzy type......ULIMBUKENI TU. HONGERA DIDA. MUNGU AKUPE BARAKA ZAKE UDUMU KATIKA NDOA HII.

      Delete
    2. Huyo mgalatia unayemtaja kwani alimlazimisha Dida amuoe??? Hebu achene dharau kama mnajuwa kuwa wagalatia wanatia dhambi kwanin mnakubali wawatongoze?? au kwa nini mnawatongoza???

      Kwenda zako mnafiki mkubwa wewe kazi yako kupandikiza chuki za kidini hata pasipo hitajika hizo chuki za kidini. Hivi kwanini watu wengine muda wote mnatamai ugomvi tuuuu???

      Tumeshuhudia ndugu zetu kibao wanaoan waislam na wakristo na ndoa zinadumu mpaka vifo vinawatenganisha na hakuna maswala ya kutiana dhambi hapo kama ndoa imevunjia haikuwa riziki na sio kisa mgalatia je sisi wagalatia tuseme kuwa Dida ndo alikuwa anamtia dhambi G????

      Usipende kujudge na kuona kuwa dini moja ndio iko sahihi na nyingine ni dhambi, kama limetokea tatizo na wametengana na Dida kapata mume mwingine tusianze kutafuta nani mwenye kosa yaliyopita si ndwele tugang yaayo sawa??? wewe chaumbea na kizabi zabina

      Delete
    3. Anony hapo juu umenena kwa lugha ila nasikitika pamoja na kumuelimisha huyo mwenye chuki ya kidini ubongo wake umeganda ni kazi bure. Tusonge mbele hapa ni peace tu mwache na kijiba chake akalale nacho mpaka kifo.

      Delete
  5. Mashaalwah mmependeza .Nianza na Ezden mke umepata wote mkiwa na umri mdogo nawaombeeni kheri na baraka nyingi ziwashukie mpendane ,mbembelezane, na mvumiliana mvumilie mkeo kwa yake naye akuvumilie Dar ni jiji la dhambi na thawabu fumba macho kama ulivyofumba ukamchagua Dida .
    Dida mume umempata jinsi alivyo naamini wengi wameumia mashaalwah sasa kitako mtulize muenzi na mweleweshane

    tunadumu ktk ndoa kwa kuelimishana tu mie mwaka wa 10 ,tukikoseana tunamaliza marafiki si watu

    MOLA AWAPE NYUMBA NJEMA YENYE FARAJA WANAONGOJA KUSIKIA KUTENGANA KWENU MOLA AWAUMBUE MZIKANE ,AWAPE UMRI NA KHERI KTK NYUMBA YENU

    ReplyDelete
  6. NICE COUPLEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  7. Wewe unayesema mgalatia una maanisha nini mbona mnapenda sana kuwasimanga wakristo kwani wamewakosea nini? Sio vizuri maana sote tunamwabudu mungu mmoja na akuna mwanadamu aliyekamilika jamani katika hii dunia,so nyie waislam msijione kuwa n watakatifu sana kuliko wengine wakati watu tunaoishi katika hii dunia ya mungu tuko na dhambi,ni hayo tu,Dida umependeza sana mungu awajaliye maisha marefu na baraka tele..!

    Mdau Sweden

    ReplyDelete
    Replies
    1. umeona mdau hapo juu ee kwa iyo wakristo sio watu ala kwa na siku nae G akioa tutacoment vipi kwa kumuita dida nani mfyuuuuuuuuuuuuu mungu nisamehe na mwezi huu mtukufu araaaaaaaaaaaaaaaaaa

      Delete
  8. We anon unayemsema Mgalatia kwani huyo asiye Mgalatia alifungwa kamba? Si alihiyari mwenyewe? Dida ni mtu mzima ana maamuzi na utashi wake, hivyo kama alijua kuwa G si mwenziye kiimani alikuwa na nafasi ya kuikataa kabisa hiyo ndoa na wala Mgalatia asingekuwa na jeuri ya ku-force. Kumbuka katika dunia hii hakuna aliye mkamilifu hata mmoja sote tumepungukiwa.

    ReplyDelete
  9. Mgalatia? Cheza na Mungu tu utajutra

    ReplyDelete
  10. waislam wanapenda sana kukashfu dini ya wakristo sijui wamewakosea nini na mnaishi nao na wengine wameajiriwa na wakrisho mbona hawaachi kupokea mshahara? na hela hiyohiyo ananunua ftari na imetoka mgalatia. mshuuuuuuu! shuwainii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tuweni wapole na wenye akili msibishane nao

      Delete
  11. Mgalatia shangazi yako! Hovyo we nani alikudhihirishia hiyo dini yako ndiyo ya kweli? NDIYO MAANA MWEZI WA RAMADHANI NYAMA YA NGURUWE HAINA SOKO. JIULIZE KWA NINI JIBU UNALO!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kula 5 mdau nimekuLOVE gafla:)

      Delete
  12. jamani watu wengine muwe mnaangalia maneno ya kupost ,dini zote tunamtukuza mUngu haya mambo ya Ubaguzi wa dini wapi na wapi?

    Dida muwe na mfungu mwema

    ReplyDelete
  13. Muulize huyo anayeita wenzake wagalatia.

    ReplyDelete
  14. kwani hamjui kilichowakosesha shule? akili ya kufikilia kichwani mwao uwa hakuna, kazi yao uwa kuropoka tu bila point, wanawachukia wakristo kwa sababu wanawapelekesha kwa elimu, sasa wanashindwa jinsi ya kujibu mashambulizi kisomi wanaishia kuropoka na kutukana matusi yao yale ya uswahili, kwi kwi kwi, chezea elimu wewe!!mtabaki hivyo hivyo na vichwa vyenu vigumu visivyoenda shule, sisi twapeta tu. waislam mnachekeshaga nyie. nendeni shule bwana.

    ReplyDelete
  15. Jamani tujaribu kuwa waelewa kdg basi, ni kweli iliposema mgalatia kamaanisha mkristo, nå ni kweli kwa misingi ya dini ya kiislam hakuna ndoa Kati ya muislam nå asiye muislam, watu wanalazimisha TU,ndio maana mtoa maoni hapo juu akasema walikuwa wanapatishana dhambi, especially kwa upande wa Dida alie muislam, khs upande wa dini yenu cjui sheria zenu zilivyo....
    Helper.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na mke wa mtume Mohamed mmoja alikuwa dini gani? Acheni hizo someni vizuri hiyo Quran yenu tatizo lugha hamuijui mmefungwa tu mnafata upepo basi. Hiyo Quran siku mkiisoma mbona mtafunguka mko gizani.

      Delete
    2. Kama hujui sheria za kikristo mbona mnasema alimpatisha dhambi? NB:Sisi tunaangalia usafi wa moyo na si wa nje,Heri wenye moyo safi maana...............

      Delete
    3. Sisi hiyo quran inayoisema WW tumeshaisoma nakuielewa vzr tu, kama unaona haijaeleweka basi tutafsirie WW unaeijua ili tuelewe.....imekushinda kuielewa biblia ambayo inakuhusu utakuja kujua Quran??!
      Helper

      Delete
    4. Nimesema anampatisha dhambi kulingana nå sheria zetu sisi ninazozijua, Yeah za kwenu hatuzijui so cjui kama kwenu inakubalika au hapana ila kwa upande wetu ni dhambi.
      Helper

      Delete
  16. Waislam ni wabaguzi sana.ila asante Mungu wakristo ni watu wenye busara sana.Mungu aliumba wakristo na waislam kwa makusudi,wote ni wakwake.kila Mtu ataiona pepo kutokana na matendo anayotenda na si vinginevyo. na Mwenye kuhukumu ni Mungu peke yake co mkristu wala muislam.Africa dini zimeletwa tu.

    ReplyDelete
  17. Hongereni waislam wenye dini safi ila kitimoto mbona tunakula wote? Yaan mnapenda sana kusema wakristo kosa lao nn?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Walio waislam safi hawali kiti moto, ukimuona anakula basi muislam kwa jina tu sio matendo.....halafu ukiangalia comment zooote aliesema wakristo nani? Mbona mnajishuku sana, alietaja khs ukristo mmoja tu, BT mliojibu hamna idadi kuonesha jinsi gani mioyo yenu Haina amani nå dini za wenzenu.....jibuni tena nå hii

      Delete
    2. unafiki tu huna haya mwana izaya wewe kujiita msafi wakati pua zako zinaangalia chini. Mwenyezi Mungu ndio msafi pekee tena koma ukomae we bin-adamu kujiita msafi wakati bado uko safarini na unaishi dunia hii kwa kudra za mwenyezi. Ni Mola pekee mwenye haki ya kusema yupi msafi na yupi siyo.

      Delete
  18. dida mmependeza sana wewe mumeo...heri ya ramadhani,kumbe nguo hizinakutoa sana..Dada Lillian Ericksson

    ReplyDelete
  19. Amemsema G ambaye ni mkristo. Na kwa taarifa yako wewe mdau hapo juu asilimia kubwa ya waislamu tunakula nao kitimoto kwa sana. Na sasa hivi baa za kitimoto nyingi hazina wateja hadi mfungo uishe mpaka wenye baa wanalalamika.

    ReplyDelete
  20. hongera sana na mungu azidi kuwasimamia inshallah!!

    ReplyDelete
  21. mi nadhani kuna kutokuelewana hapa kwani ndoa aliyofunga na G ilikuwa na bomani kwenye uislam haikubaliki na walikuwa wanahesabiwa wanazini siku zote walizoishi, kula nguruwe ni utashi wa mtu na sio ndio msahafu umehalalisha, ye dida anafahamu kama alitoka nje ya dini yake, pia mambo yote tunaweza kushirikiana lakini kwenye ndoa, maziko na mazazi kila mtu anafuata utaratibu wa dini yake

    ReplyDelete
  22. Uislam unaruhusu mwanaume wa kiislam kuoa mwanamke wa kikristo but si mwanamke wa kiislam kuolewa na mkristo though kidunia tunafanya hivyo
    Pia uislam unasema hamna mtu mwenye dhamana ya kukosoa na kukashifu dini ya mwingine. ... muislam kasome sura inaitwa ....araitalladhii yukadhiibu bi ddin na tafsiri yake then uache kukashif na kukosoa fini ya mwenzio wuran tukufu imekataza

    ReplyDelete
  23. dida nialike basi na mimi kwenye futari

    ReplyDelete