Kitabu cha Werrason

Monday, April 23, 2012 1 Comments

Werrason ni mmoja wa wanamuziki wa Congo wenye washabiki wengi sana hapa nchini na Africa  na Duniani  Lakini kwa muda mrefu mashabiki na wapenzi wake hao wamekua wakimfahamu Le Roi De La Forret Papaa na Exocee Mobali ya Mama Pastor Sylvie Mampata kijuu juu tu. Lakini
safari hii mashabiki wake na wa muziki kiujumla hususan wanafamilia wa
wenge wamepewa fursa maalum ya kumjua nguli huyu wa muziki wa congo
kupitia kitabu mahalamu ambacho kimeshachapishwa kikielezea historia ya mwanamuziki huyo binafsi na katika harakati zake za kujiingiza kwenye muziki, kuwa star na mpaka sasa kumiliki bendi kubwa na yenye
mafanikio makubwa .

Dondoo za yaliyomo kwenye kitabu hicho ni kwamba ndani ya kitabu hicho
werrason anaelezea kwa mfano wenge musica ilivyozaliwa. Katika hilo
Werrason anasema mwanzoni kabisa walikua yeye Werra, Aime Buanga, Jean Belix Luvutula, Didier Masela na Christian Zitu, ambapo Aime Buanga
alichukuliwa kama muanzilishi wa kundi kutoka na yeye kujitolea nyumba
ya wazazi wake alimokua akiishi itumike kama sehemu ya kufanyia
mazoezi ya kundi lao hilo na pia Didier Masela nae kwa upande mwingine
akichuliwa kama muanzilishi pia kutokana na kwamba wazo la kuanzisha
bendi lilitoka kwake

1 comment:

  1. VIPI JB MPIANA INA MAANA SIO MUANZILISHI WA WENGE MBONA MWANDISHI HAJAMTAJA WAKATI NDIO ILIKUA NEMBO YA BENDI

    ReplyDelete