TUSAIDIANE WANAWAKE KWA HILI SABABU YAPO SANA BONGO.
Namshukuru sana mwenyezi mungu bado anaendelea kunipa pumzi,Kuna dada alinitumia msg nimsaidie ushauri toka ameolewa ana miezi kama minne hivi ila kuna mdada anamtumia msg za matusi sana na kumwambia atahakikisha anamchukulia mumewe na mambo mengine mengi ameomba niweke kwenye blog ila tumsaidie hata kwa mawazo anampa kashfa nyingi sana so karibuni ila naomba nianze hapa juu mie wengine tuta comment.
dida said
Mimi nakushauri dada usijali,na kuwa ngangari kwenye ndoa yako hao ni wanawake tu wapo kwa ajili ya kukukosesha raha mjini jua anayetaka kuchukua cha mtu hatangazi yeye tu kwa raha zake na usikose usingizi kwa mtu ambaye bado mpk sasa anangoja kutafuniwa yeye ale ila cha mwisho si kila mwenye ndevu ni za bahati wengine za mkorogo,asikuumize kichwa bora wewe upo kwako kackuchagua yeye ataendelea kumsubiri uchochoro ang"atwe na mbu atoke @ yahoo.com miguuni wewe ndio mwenye hati miliki asikupe vipele vya joto wakati kuna dalili ya mvua.
Dida bwana!
ReplyDeleteHuo ni ushaurii!!! au mipasho? kha! inaelekea mtoto mswahili sana wewe!! nakushauri mtu akitoa shida yake anaomba ushauri itume mail yake tuione alivyojielezea ila mail address ficha tu, hapa mi naona kama unatoa yako ya moyoni tu, unasema wanangojwa vichochoroni??? Hotel ambazo wewe hujawah kanyaga kama mke ndo wanapelekwa wenzio.
Haya ushauri kwa dada namba zote zimesajiliwa amsake tu hata kama hajasajili bado ana uwezo wa kumjua ni nani na anaishi wap afanye tu halafu polisi watamsaidia kumalizia kazi.
namshauri aachane na huyo mtu asimjibu wala nini, km anapendwa kwanini hakuolewa yeye?tulia ishi na mumeo kwa amni na upendo inshaallah allah atawaepusha na kila baya.
ReplyDeleteMARIAM
habari da dida minakupenda sana kwa kuwa unaongea ukweli kila siku mwambie huyo dada asiwe na wasiwasi kwani mwanaume ndio wa kwanza kutangaza habari za kuoa na si mwanamke kama anavyojiashua mi mwenyewe wapo kibao wanaonisumbua jibu linalowapa ni kama anakupenda akuweke hadharani na si kukuficha kama damu ya mwezi siri moyoni mwako.asante da dida- naitwa ramla au mama najma ukipenda mrs shabani
ReplyDeleteShalom dada yangu mpendwa.
ReplyDeleteKwanza pole sana kwa kupata jaribu kwenye ndoa changa. Hata mie nilipoolewa kuna mwanamke alikua ananitumia sms mbaya mno na nyingi mno za matusi na kashfa nzito hadi nikashangaa ila kuna mtu mmoja akaniambia usimjibu chochote na wala usibadili namba yako ya simu. Alinitukana kama miezi mitatu usiku na mchana na mie sikuwa najibu wala kusoma chochote, nilikua nikiona namba ile nadelete zile meseg bila hata kuzisoma. Ushauri wangu kwako ni kua usisome hizo meseg wala kuzijibu. Nyamaza kimya mami na baada ya muda atachoka mwenyewe. Usimtie moyoni wala kumuwaza huyo anakutishia tu hana la ziada. Hakuonekana hadi wewe ukaolewa? Achana nae na wala usimuwaze hata kidogo.