NAWASHUKURU WOTE MADADA NA MARAFIKI ZANGU WOTE MLIOHUDHURIA KWENYE KITCHENPART YA DADA YANGU ALIYE NILEA TANGU MDOGO NAWASHUKURU SANA.

Sunday, November 07, 2010 31 Comments

Felista na matron wake wakiingia ukumbini.
Bi shost nilipotunzwa mijihela.
Nawashukuru kwa mkwanja.
Mhhhhhhhh.
Hawa ndio mashauzi famili ikiongoza na isha mashauzi.
isha akiniambia kitu du pembeni ni mc kiatu.
Jamani kupendana raha hawa ndio mashauzi family.

Dada yangu wa ukweli akinitunza ni mc hidaya njaidi muigizaji filamu maarufu tz.
Bi hindu akimpa maneno mawili matatu bi harusi.
Tukimkabidhi kabati.
Dida na isha mashauzi.
Isha alituchesha kiukweli inatia raha na wala si karaha ana vipaji vingi.
Rose jimama akifanya vitu vyake mwanamke nyonga makalio hata mbwa wako anayo.

Tulicheza baikoko live.

31 comments:

 1. kaz mnayo wanawake wa uswaz hata kama mnakaa masaki or wherever tabia zenu za kiswahili mno mnanichefua kweli

  ReplyDelete
 2. waooh hongereni sana ilipendeza mno.kuishi na watu vizur ni raha jaman.tunaomba utuwekee wimbo wa domo kaya wa jahazi modern taaran,pls tupo majuu thhen huo wimbo haupo ktk web.nilikuja mara moja nikauskia nikaupenda,kaimba kijana mdogo.

  ReplyDelete
 3. DUNIA TAMBARAREEE LOL........

  ReplyDelete
 4. Jamani we dida huyo ndugu yako hata maznat saloon ambayo kidogo unaweza pambwa ukapendeza hukumshauri akaenda kajitwika mnanasi huo juu umepitwa na wakati mbona kama washamba yle mie nakuona we wa mjini na huyo isha anauza hilo duka shilingi ngapi miziwa utadhani kapewa tenda ya kunyonyesha watoto yatima loh mjiangaliege maumbo yenu ndio mchague nguo za kuvaa otherwise mwageuka vituko.ni hayo tu kwa leo hata ukishushua ukweli ndio huo na habari ndio hiyo.mashauzi family mnayaweza hela zenyewe hamna mnajishaua tu tena bora hata we dida mwanamke mhangaikaji nakukubali sana ila hao wengine sina hakika nao.then mbona picha za vyombo hatuzioni au ndo sahani na bakuli mbili hicho kikabati cha dubai ndo nilichoona cha maana kama kuna nyingine weka tuone mana hiyo ndo maana ya kitchen party

  ReplyDelete
 5. RAHA JIPE MWENYEWE! NA HIYO SIKU YAKE LAZIMA AFANYE KILE ANAJISIKIA YUKO HURU NACHO, KAMA KAPENDA STYLE HIYO WALA SIMLAUMU, NI MAPENZI YAKE!! SI KILA MTU ANAENDA NA LATEST STYLES, USIISHI KWA AJILI YA WATU, ISHI KWA AJILI YA NAFSI YAKO. WAJA KUSEMA NI KAWAIDA!!!!!

  ReplyDelete
 6. Hata hamkupendeza, majigambo mengi bure.

  ReplyDelete
 7. pendezaa sana nyie.

  ReplyDelete
 8. we dida hivyo viatu si vya baridi?

  ReplyDelete
 9. dida mbona watu wanapenda kukuponda sana?walimwengu acheni chuki na mwana wa mwenzenu,mara hoooo mnajishaua hela zenyewe hamna jamani kwani iyo kitchenpart uliifanya ww?watu midomo mmepewa na dida kweli unawapa wakati mgumu hasaa wanaokuchukia kitu kidogo washapayuka,mambo yakitchenpart ya dadayake pia yanawauma?mhhhhh kazi mnayooooooooooooooooooooooooodida wachomeeeeeeeeeeeeeeeee

  ReplyDelete
 10. make up jamani make up muambiweje kiwaimgie kiwakune HAMPENDEZI KAMA VINYAGO HATA VYA MPAPURE VINA AFADHALI KHAAAA KINYAAAAAAAAAAAA

  ReplyDelete
 11. mhhhh hizo make up mnatisha, kila mmoja anamshinda mweziwe kazi kweli kweli

  ReplyDelete
 12. Dida naomba undugu kwenye mashauzi Family nimeipenda iyo

  ReplyDelete
 13. ongereni,lkn mbona zawadi amjatuonesha zote,ukiyavulia maji nguo sharti uyaoge tuonesheni na vingine zaid ya ilo kabati babu,aihuuuu!

  ReplyDelete
 14. huyo bi harusi mbona kama kapakwa utomvu wa fenesi huko machoni? imekuaje?

  ReplyDelete
 15. Dida wewe ni binti mzuri sana, na umelelewa na mama yako vizuri, lakini hicho kikundi cha MASHAUZI kinakushusha hadhi hakikufai wewe huko juu. ACHANA NA HAYO MAJIMAMA NA MIMWANAUME INAYOJIFANYA WANAWAKE yaani WA.EN.E maliza mwenyewe

  ReplyDelete
 16. Dida wambie wenzako wasichezee FEDHA kwa kujishaua kunatisha pesa ni uaribifu acheni michezo ya kijinga kama hiyo kama wanataka kukutunza mwenzenu wekeni kwenye bakuli kisha ziesabiwe

  ReplyDelete
 17. ai,huyo bi harusi kazubaa kama viazi mbatata kwenye pilau,na huyo isha mashauzi ndo minywele gani hiyo,naye anajishaua kama vitunguu saumu kwenye pilau anataka aonekane yeye tuu,kama vitunguu saum vinavyotaka kusikika vyenyewe tu kwenye pilau lol.mwatiilishaaaa.

  ReplyDelete
 18. Kujishaua koooote zawadi ya kichina!!Lol.

  ReplyDelete
 19. dida tunaomba utuwekee mwimbo wa isha mashauz wa tugawane ustaarabu,upload plzzzzzz nampenda sn huyo dada...

  ReplyDelete
 20. Jamani kwakweli uyo bi harusi hata hajapendeza jamani, nini sasa kapaka huko machoni, hapana kwakeli lol..

  ReplyDelete
 21. kila mja hufanya kitu chake kwa uwezo wake na anaruhusiwa kujiachia atakavyo,nawashangaa mangurumbembe acheni wivu kizuri kisifieni na kama kunasehemu wamekosea kuna jinsi ya kumuelimisha mtu.

  wewe unayesema bi harusi kazubaa wewe una achari machoni?

  wewe unayesema hajapendeza harusi yako ilikuaje?

  wewe unayesema wanajishaua na kikabati cha mchina na pia hela hawana hivyo waache kujinadi,wewe hujawahi tunza kwa rusha roho ki kanga cha india kimoja na sahani za buku za mafungu tena ukalia?

  acheni kejeli,kumbukeni ASIYEUMBA DAIMA HAUMBUI.hebu waacheni wale mananasi yao kwanafasi.

  mama Rique.

  ReplyDelete
 22. wote mliotoa kashfa nyumba zenu zinawaka moto kwani mnaonekana mna nongwa sana,mnaboa.

  ReplyDelete
 23. dida siku nyingine bi harusi mpeleke kwa maznat akarembwe zaidi,sisemi kwamba bi harusi hajapendeza ila ili awe tofauti zaidi basi mpeleke huko.

  otherwise mmejitahidi sana,big up.

  ReplyDelete
 24. kama viatu vya dida ni vya baridi,je mbona madukani vyauzwa au bongo kuna snow zinadondoka kipindi chake kikifika?acha roho ya kwanini utakua hufanikiwi mzazi.

  kama nywele za isha ungezipata wewe ndo ungekua kwenye fashion?she is beuty bila hata hizo nywele ,do ur things let isha does her interest hata akitaka za njano ni yeye we zako za pink zi wapi?acha kashfa maisha mafupi na yana kujichakachua.

  mrs salim

  ReplyDelete
 25. mhh pole Dida kwa kuweka hizo picha. Kushambuliwa koooote huko pole bin dada

  ReplyDelete
 26. dida mimi nitakutafuta kwaajili ya baikoko jamani naipenda kweli ngoma yangu ya tangaa mambo ya leso hehehee

  ReplyDelete
 27. kama huyo dada alikulea anaolewa leo sasa ana miaka mingapi jamani, na wewe ndio ushakuwa shangingi maarufu DAR

  ReplyDelete
 28. kweli aloimba uswahilini kuna vituko hajakosea!! hapo alopendeza ni Dida tu,wengine make up utazani majivu! halaf jamani kwanini tusiangalie maumbo yetu tunapoamua kuvaa? kila mtu anauhuru wakuvaa atakacho sikatai,lakini kweli tujiangalie kwanza tukoje!!

  ReplyDelete
 29. Dida, Neno langu liliwachoma hadi mmeamua toa comment yangu?
  ila nashukuru..hii inamaana ujumbe ulichoma mahala husika
  sikusema kwa ubaya, ni kupeana tu mawaidha, ndio maana tuna vichwa hadi mighuu.
  tusiporekebishana humu, wapi tena?

  ReplyDelete
 30. hao wanaoleta hivyo viatu bongo washamba ss huku tunavaa wakati wa baridi ikiisha tunaweka stoo,winter mpaka winter.muulize dida joto lake alilionaje?

  ReplyDelete
 31. jamani hvo viatu ni vya kipindi cha winter, hata msipokubali habari ndo hiyo

  ReplyDelete