Mgomo wa mafuta ni nouma Dar!

Thursday, August 04, 2011 1 Comments

Siku nzima ya leo jijini Dsm na miji mingine tangu asubuhi kumekuwa na mgomo baridi kwa wauzaji wa mafuta especially Petrol na Diesel, ambapo vituo vingi vya mafuta vimekuwa vikidai kuwa mafuta yamekwisha na kusitisha huduma hiyo wakati ukweli ni kwamba WAMEGOMEA BEI MPYA YA MAFUTA HAYO ILIYOTANGAZWA KUANZA LEO

Magari yakichomoka petrol station baada ya mafuta kuisha

Mida hii ya saa saba za usiku, hapa natokea kituo cha mafuta cha Victoria huku nikiwa nimekosa mafuta kwa ajili ya gari yangu baada ya kusota kwenye foleni kwa masaa kadhaa. Kituo hichi ni moja kati ya vituo vichache sana vilivyokuwa vikiuza mafuta kwa siku ya leo na kufikia saa hizi mafuta yalikuwa tayari yamekwisha kisimani huku magari kibao yakibaki kwenye foleni.




foleni ilianzia barabarani kuingia station



unaweza kudhani ni foleni ya trafic light.....


1 comment:

  1. Hiyo ndo Bongo,mbona bado mpaka 2015!Hiyo ndo Bongo,mbona bado mpaka 2015!

    ReplyDelete