Hongera Machozi Band kutimiza miaka sita.

Monday, July 25, 2011 1 Comments


Ijumaa iliyopita ya tarehe 22 Binti Comandoo na Bendi yake ya Machozi walitimiza miaka sita (6) tangu kuanza kwake,
wamepitia mengi magumu na mazito na kwa support ya Fans na discipline ya wanamuziki wenyewe wamefikia hapo....
Hongera sana kwa Uongozi wa Machozi Band kwa ukubwa mliouonyesha na heshima pia kwa wapenzi wa burudani hio kupata Tuzo.

Kutambua na kuthamini mchango wa wanamuziki na wadau waliokuwa na sisi tangu tunaanza hadi leo, tuliamua kutoa Tuzo kuwashukuru kwa mchango wao.

Pichani juu Ni Mwinyi Goha, akikabidhiwa tuzo ya Mwanamuziki anejipenda na mwenye muonekano Safi, kuanzia mavazi n.k kwa kipindi chote ambacho yupo kazini.
Swahiba, Shamim Mwasha akimkabidhi Mbwana Mponda Tuzo ya Mwanamuziki aliekaa na Band kwa muda mrefu kuliko wengine wote.
Huyu anapiga Bass Guitar, Tangu MACHOZI inaanza mpaka leo yupo

Jonico Flower, Best Vocalist hilo halipingiki hata Jide anaweza kusubiri hapa

Mfanyakazi Bora alikuwepo lakini alikuwa kazini hakuweza kuinuka hata kuifuata Trophy yake, mkewe akamchukulia akampelekea pale alipokuwa amekaa
Huyu si mwenye Tuzo, ni mke wa mwenye Tuzo hiyo inayoonekana pichani juu

Baada ya kupokea kikombe na bahasha ya fedha taslimu alienda kuzikabidhi kwa baba kwanza, zikatiwa barka halafu kama ma mwenye nyumba akarudi nazo kuzimiliki na kuzipangia budget
Mfanyakazi bora wa MACHOZI BAND anaitwa DUDU
Best Male Supporter "ERASTO LUGENGE"
Pamoja na kuwa tunaimba watu wanakuja, lakini kuna watu huwa wanakuja kila siku, lije jua ije mvua na tumetambua mchango wao.

Best Female Supporter "TINDWA"
Tangu Chozi linaanza JJ Blue mpaka linapata makazi yake Nyumbani,
mdau yupo tu

BLOG HII INAWAPONGEZA WASHINDI WOTE WA TUZO HIZO NA KUWATAKIA KILA LA KHERI KTK KUENDELEZA BENDI YA MACHOZI


tembelea zaidi
http://ladyjaydee.blogspot.com/

1 comment:

  1. JAMNI TUACHENI UTANI HUYO JAMAA ALIE VAA SUTI NYEUPE ERASTO PICHA YA PILI TOKA MWISHO AMEFANAN SANA NA MAREHEMU MPKANJI AU MNASEMAJE

    HAHAHAH DIDA HONGERA KWA HARUSI ILA UMEVAA KIZAMANI SANA YANI UTAFIKIR P[ICHA YA 1996 HILO VERY HAHAHAHAH NICHAMBE TU UJUMBE UMEKUFIKIA

    TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI ILA JAMAA MHH UMECHAGUA BONGE LA DUDE ALAFU KIJANA HALOOOOOOO

    KISHUNA

    ReplyDelete