SIPENDI WANAWAKE MNAOWANANGA WAUME WA WENZENU TUONYESHENI WENU JAPO KWA PICHA.

Wednesday, November 03, 2010 18 Comments

WAPO WANAWAKE WALIOKOSA KAZI NA KUANZA KUWACHAMBUA WAUME WA WENZAO, jamani embu tupigieni picha waume zenu tuwaone mara mume wafulani mbaya ubaya wake anaubeba mgongoni?mara oooh mnene kampenda yeye wewe inakuhusu nini?mara kaolewa na mtoto mdogo una kadi yake ya kliniki na mbona akienda toilet anaufunga mlango na asiuwache wazi?umbile si hoja hoja virutubisho udogo wake kwa wazazi wake, mara mumewe mkubwa anaogea ikulu na huo ukubwa alionao hamjui kuwa ng'ombe hazeeki maini?acheni hizo jamani mume kila mtu anapangiwa na mwenyezi mungu na wale wanaozungumzia wenzao wameachwa cha ajabu kipi kaachwa mama winnie mandela na dunia nzima ikajua msiwachoshe na wala msichoshane kwa maneno hata kwenye keki yapo, sembuse wengine acheni midomo wazi kama milango ya jela hajatajwa mtu jina ukijishuku lako.

18 comments:

 1. LEO KIDOGO UMEONGEA KITU CHA MAANA, WENGINE UTASIKIA OOH KAOLEWA NA MTU HANA PESA WAMEKUJA KUOMBA UGALI KWAKO KUPATA NI MAJAALIWA NA KILA MTU NA MAISHA YAKE WAJA

  ReplyDelete
 2. tenaaaaaaaaaaaaaa maneno kuntu baelezee bajue

  ReplyDelete
 3. Dida wachomeeeeeeeeee,wachomeeeeeeeeeeeeee hahahaaaaaaa hilo nalo neno,tupa mawe gizani mama atsakaesema aiiii ujue limempata

  ReplyDelete
 4. he he he heeeeeeeeee mbavu zanguuuuuu!!!!!
  Dida weweeeeeee hujatulia... umenivunja mbavu zangu nusu nijikojolee.
  Ashurah H

  ReplyDelete
 5. Haswa waambie hao Dida umenikuna wengine wanaona fahari eti ooh kaachwa mie nitaolewa bomani hajui kuiba mume wa mtu ipo siku kikaango kitageuka kwako hembu nipe neno kwa wale wanaojiona wamefika kuchukua waume za watu horiyaaa tenaaqa

  ReplyDelete
 6. Dida ubaya wake haunihusu bibi baelezeee baelewe mamamamamamae

  ReplyDelete
 7. Kula 5 bibi siiiijui kwani haipiti utoto angenifuata watupisheee tena km treni ikipita

  ReplyDelete
 8. Dida ukiwachunguza hao wanawananga waume wa wenzao wengi wao ni Manungayembe,ambayo hata hayajawahi kunusa harufu ya ndoa,halafu uwa hawana lolote wanawatamani ndo maana wanasumbuka kuwachambua,na kuachwa wala si ajabu,kuna wengine wamo tu kwenye ndoa ndoano heri alieachwa, wengine mume hamjui kwa zaidi ya mwezi,wewe nawe utacheka alieachwa?kuna mwana fulani huku Mwanza kazi yake kuchongoa mdomo kwa ya wenzake,ya kwake tunayajua sana tuuuu,mume miezi 3 humjui,nawe unajinadi MRS mara MAMA .....unachekesha sana wewe bi kizee.

  ReplyDelete
 9. wangu mfupi basi sipumui jamani!! bora umewafungashia ukawarushia kazi kwako...atakaye daka lake hilo

  ReplyDelete
 10. jaman yan huwa wananikera kweliiiii....hao wanaosema mbaya ndio hao hao wanakuja kukuibia mume...niacheni nimempenda

  ReplyDelete
 11. binam safari umenitolea mbukwa, looo..!! umenikunaje..!! basi hao wakuwananga waume wa wenziwao, wao hata wakuwaambia mwenzangu basi njoo tuanze maisha hawana, akikutana na huyo mume wa mwenzie njiani shem naomba lift au kwenye baa 'shem naomba ninunulie bia moja'.. inahuuu!!!

  ReplyDelete
 12. shosti sikuwezi kabisa,
  maneno hayo nimeyapenda sana na msg delivery kabisaaa bila chenga.
  nimecheka mpaka basi yaani narudia kusoma mara mbilimbili hapa.

  ReplyDelete
 13. ktk siku uliongea maneno ya maana basi ndo leo jamani unapomnanga mume wa mwenzio wako kakamilika hauwezi jua wamependaniana nini halafu usimzodoe mwenzio kisa kaachika hakuna mtu anayependa kutoka ktk ndoa yake ikifikia hatua akaamua kubwaga manyanga ujue kafika point of no return kwa hiyo ulitaka aendelee kuishi maisha ya kumnyima raha kisa asisemwe kaachika waja muwe na uelewa aliachika malikia cleopatra mrembo wa misri aliyevunja rekodi dunia nzima kwa uzuri wake utashangaa nini kwa mwingine keep it up dida

  ReplyDelete
 14. kwa mara ya kwanza umeongea point. uzuri wa mtu upo machoni pa mtu. kila mtu na chaguo lake usimlazimishe mtu achague mtu umtakae ww. mfano wadada wa ss hv wanaonekana wanbabaikia wanzungu mm jamani na mwanaume mweupe tofauti kbs awe mzungu mwafrika au mwarabu. ila siwalaumu maana ndio machaguo yao na wala siwezi kuwaponda. uzuri wa mwanamke au mwanaume unaliwa, cha muhimu ktk maisha ni upendo wa dhati na km mtu umempenda huwezi kuziona kasoro zake za kimaumbile. ss wakristo tunaamini kuwa tumeombwa kwa mfano wa mungu
  mimi wangu ni mrefu halafu amejazia na mnene kiasi mm mwenyewe ni mdogo mdogo basi nasemwaje ohh kaolewa na jitu zima, ohh kaolewa na baunsa, ohh mara mwanaume kuna siku atanivunja, yaani wala siwajali, mm na mwanaume mdogo mdogo tofauti kabisa maana wanawake mara nyingi tukizaa tunaongezeka. yaani watu wanamenono, serikali ikiweka luku kwenye midomo halafu itoze VAT watu watafilisiwa mali kwa kudaiwa kodi

  ReplyDelete
 15. WAAMBIE BWANA WAELEWE KWANI KUNA WATU WANAPENDA SANA KUWANANGA WANAUME WA WENZIO. MARA UTAWASIKIA JAMANI MBONA MZURI KWA NINI UMEENDA KUOLEWA NA YULE MZEE. NYIE INAWAHUSU NINI?

  ReplyDelete