JOMO KENYATTA AIRPOT YAWAKA MOTO

Wednesday, August 07, 2013 0 Comments

Kwa habari zilizotufikia asubuhi hii ni kwamba Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) umeshika moto na kupelekea kusimamishwa kwa huduma zote za ndege zinazoingia na kutoka uwanjani hapo.

Moto huo unasadikiwa kuanza  majira ya saa 10:30 alfajiri ambapo Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Ndani nchini humo Bw. Mutea Iringo anaratibu shughuli zote na kuhakikisha wanapambana na kuuzima moto huo.

Mpaka hivi sasa hakuna mtu yoyote aliyedhurika na moto huo.

0 comments: