O'NEAL AMKOROMEA FEZA BBA BAADA YA KUOGA NA MWANAUME MWINGINE

Thursday, July 18, 2013 2 Comments

Wakati shindano la Big Brother The Chase linapamba moto na maswali yakiendelea kuzunguka vichwani mwa watu juu ya ni nani ataweza kuondoka na mkwanja wa millioni mia tatu, Mshiriki wa kike anayewakilisha Tanzania Feza Kessy asubuhi ya leo allijiwashia moto kwa mpenzi wake pale alipoanza kuulizwa kwanini ameoga na mwanaume mwingine tena mwanaume huyo akiwa uchi kabisa…!!!

Feza akiwa O'Neal wa Botswana...
 
Tukio hilo la kuoga halikuonyeshwa lakini ikaja kuonyeshwa hiyo sehemu ambapo O’neal a.k.a Bwana Shemeji toka Botswana akimgombeza Feza kwa kitndo hicho ambacho ni mara ya pili karudia.


Feza alijaribu kujitetea na kusema hakukua na chochote kilichofanyika, Oneal akamwambia what if Tanzania ikitumia picha yake na mwanaume huyo ku-publish story kitu ambacho kita-discredit mahusiano yao…Ndipo Feza akaomba msamaha kwa tukio hilo na kusema haita tokea tena, na O’neal amemsamehe…. Life goes on in the Big Brother Africa…

2 comments:

  1. Kiukweli Oneal anampenda sana ndugu yetu ila duuu huyo dadaetu sasa, snitch wa nguvu, kama ni game basi shosti anajua kulicheza tatizo sometimes anaharibu kama sasa hivi hadi anaifanya nyumba ya Ruby inabore kutazama, kwanza kupika hajui, akipika anapika cha yeye na bwanshemeji tuuu wakati wenzie wanapika cha wote na hadi kupakuliwa anapakuliwa, ana kachuki binafsi kwa Pokelo wa Zimbabwe, nguo hana maskini, lakini all in all ni wetu tutampigia kura abaki mwanzo alicheza vizuri sasa hivi anaharibu

    ReplyDelete
  2. OK SIE TUPO KUPATA KINACHOENDELEA MAPENZI YA BBA NI YAKUPITA TUU KWANI WANAACHA STORY T LAZAIDI HAKUNA .

    ReplyDelete