MANDELA ATIMIZA MIAKA 95 AKIWA HOSPITALI LEO
Siku
ya Mandela huadhimishwa kuenzi kazi za kiongozi huyo alizozifanya kwa miaka 67
akiutumikia umma wa wananchi wa Afrika Kusini, zikiwamo vita dhidi ya ubaguzi
wa rangi na hatimaye kuwa Rais wa kwanza mzalendo kwa miaka mitano, kisha
kustaafu.
“Happy birthday Mzee Madiba.” Rais wa kwanza
na mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, leo anatimiza umri wa miaka 95,
pia anatimiza siku ya 40 tangu alipolazwa katika Hospitali ya Medclinic,
Pretoria kwa ajili ya matibabu.
Nelson
Rolihlahla Mandela, alizaliwa Julai 18, 1918 katika Kijiji cha Mvezo, eneo la
Mthatha, Transkei Mkoa wa Eastern Cape na ametumia zaidi ya asilimia 70 ya
maisha yake akipigania haki na usawa wa wananchi wa Afrika Kusini.
Maadhimisho
ya miaka 95 tangu kuzaliwa kwa Mandela yanabeba uzito mkubwa kuliko maadhimisho
mengine yaliyotangulia kwani kwa siku 40, wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa
katika wasiwasi mkubwa hasa kutokana na kuzorota kwa afya ya kiongozi huyo.
Mandela
alilazwa katika hospitali hiyo Juni 8, mwaka huu akiugua magonjwa ya figo na
afya yake imeelezwa kuwa ni mbaya.
Huu mwandiko sio wa dida!
ReplyDelete