MACHACHARI NDANI YA BIG BROTHER WAAGA MASHINDANO
Katika hali iliyo washtua wengi ile jana katika eviction show kule Afrika kusini ni pale jina la washiriki wawili ambao wameonekana kua ni machachari sana katika ushiriki wao mule ndani kutangazwa kua wanaaga mashindano hayo na kurudi katika nchi zao.
Mshiriki wa kwanza kutangazwa na IK kuaga mashindano hayo ni yule atokaye Ghana (SELLY) na kuna wakati alikua na mahusiano ya kimapenzi na mshiriki wa kiume toka Tanzania Nando, na hata jana wakati wa interview fupi wakati kashatangazwa tayari kuaga mashindano hayo alithibitisha kua alivutiwa zaidi kimapenzi na Nando....
SELLY wa Ghana....
Na Mshiriki mwingine kuachana na jumba la BBA jana alikua ni NATASHA a.k.a Mama Afrika ambae mara nyingi alipenda kujishughuulisha na usafi na kupika pika mule ndani, lakini sasa amerudi kwao MALAWI
0 comments: