MSANII WA TAARABU NA BONGO FLEVA HAMMER Q AMPA KIPIGO MKEWE SALHA NA KUMCHANA NA VIOO MWILINI INASIKITISHA SANA NDOA ZA SASA NI UADUI AU ?AMEMPIGA MPK KAZIMIA KISA ALIMTAMBULISHA HASSAN TX MOSHI KUWA NI KAKA YAKE IKAWA KIZAA ZAA UWIIIIII MUNGU ANISITIRI NA KUPIGWA.

Monday, April 29, 2013 30 Comments


 Baadhi ya picha za mkewe baada ya kipigooooo.


 Nguo za Hammer Q zikiwa zimetapakaa damu hatariiiii.Baadhi ya ndugu yaani ni kama msiba watu walijua kafa kabisa.

30 comments:

 1. Mtihani yarabb.Me nachukia hasa tabia hii mbaya ya kupigana hasa nyie wanaume kutufanya punching bag.Sidhani Kama mwenye mahaba hasa kwa mkewe anaweza kufanya ukatili kama huu.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Hakuna cha mitihani wala nini, sheria zote ziko wazi, za dini haziruhusu mwanamke kunyanyaswa kiasi hiki na unaruhusiwa kutoa talaka (sio kungojea upewe, unaenda kwa kadhi kama huyo msichana hapo hivyo alivyo anatoa talaka yake hapo hapo) Na kiserikali kumpiga mtu ni kosa la jinai. Kaeni hivyo hivyo Mungu nisaidie Mungu nisaidie hakusaidii ng'oo mpaka utake actions.

   Delete
 2. na wewe dida umeshaiba mume wa mtu, subiri kipigo,

  ReplyDelete
  Replies
  1. Kamuiba baba yako mzazi? Kwa hiyo unataka baba yako alale na wewe? Huna hata haya nenda kamvulie chupi wewe basi.kama huna cha kuandika sio lazia ucommet.

   Delete
 3. POLE SALHA MOLA ATAKUPA AFUEN
  DIDA NIKIWA SWEDEN NIMEKUSIKILIZA LIVE NA HAMMA Q ANAVYOOMBA MSAMAHA

  YARABII NINUSURU NA PENZI LA UPOFU NISTIRI NA WANAWAKE WOTE WANUSURU . TANZANIA KILA KITU KUROGWA SIO KWELI SHERIA ZIKO DUNI NA WANAWAKE MSIMAMO HATUNA. MTU ULIPIGWA UKAZIMIA MARA YA KWANZA TENA KABLA YA NDOA ,UKAOLEWA UNARUDIA TENA JAMANI URUMA SANA.
  PENZI UPOFU

  ReplyDelete
 4. salha mdogo wangu inatosha kama umujua mkato wa chumba sio lazma ulijue na jeneza kabla ya siku anza upwa fedheha achana nazo .Tena leo unajiuguza yy hayupo anaogopa nini Salha kilio na mwenyewe
  usikubali kuwa mtumwa wa penzi
  watu wanaolewa hata mara 100 dada .tafuta jinsi hapo hakuna kurogwa mwanaume anmkono ukirudu utakosa msaada siku yakikupata .au msamehe na mauti yanakungoja

  ReplyDelete
  Replies
  1. nakuunga mkono Salha huyo mwanaume atakupeleka kwenye jeneza hebu ona masikini ndugu zako wamejaa hapo utasema msiba mpaka watoto wanaangalia masikini umeumizwa huyo sio mwanaume Salha ondoka usimrudie leo umezimia kesho atakuuua kabisaa

   Delete
 5. Hiyo ni ndoa tukumbuke!! Kuna mapenzi katiyao ndo yaliwakutanisha kwanza,so ndugu,jamaa na marafiki nikumpa pole na si kuingilia saaaaana coz wanaodundana hivyo huwa hawaachani??? Mtakosa pakuficha sura zenu.

  ReplyDelete
  Replies
  1. inamaana dada ndoa ndio inaruhusu upigwe mpaka uzimie? acha ujinga ndoa ni mapenzi sio kupigana umenikera wanawake kama nyinyi ndio mnauliwaga kisa umegangania ndoa

   Delete
 6. Dida ndoa za kung'ang'ania hizo. Kaa kimya kesho wapo pamoja watakuchamba

  ReplyDelete
 7. pole kwa huyu dada ila aachane na hili limnyama, kama anaweza kufanya hivi anaweza akamuua kabisa siyo mwanadamu huyo. Pole mwanamke mwenzangu.

  ReplyDelete
  Replies
  1. nakuunga mkono dada limwanaume limnyama kabisaa litamuua siku yake ondoka Salha achana na myanma mapenzi hayana maumivu

   Delete
 8. Huyu ni mnyama kabisa kiukweli dida katika kitu nachukukia katika dunia hii nikuona mwanaume anampiga mkewe...mwanamke apigwi jamani...anaenziwa taratibu kunanjia nyingi zakumuonyesha mwenzio kama amekuchukiza na kitu au umekasirika lakini sikumpiga hajafanya vizuri na inaonekana nitabia yake coz nimesikilza kipindi chako na mama ake mdogo amesema ashawahi kumpiga akazimia kisa alichelewa kurudi nyumbani alitoka kwa mama ake...namshauri salha awaze mara mbili kabla ya kurudiana nae coz huyu nimuuuaji anaekupenda hawezi kuona amekuumiza akaendelea kukupiga mpaka kupoteza fahamu...anatakiwa afikirie kwamakini...wanaume hawajaisha asipoangalia mara ya pili mama yake atarudishiwa maiti...kama aliweza mpiga mwanzo akazimia sasa hivi kapoteza fahamu anatakiwa awaze mbali...

  ReplyDelete
 9. Huyu mwanamme muuaji au anamapepo,mpe pole sn huyu dada namuombea dua mungu amponye.

  ReplyDelete
 10. Nahisi huyo kaka ana pepo kwanza sura yake km mvuta bangi au amelogwa. Hapo ni ametambulishwa tu je angemfumania si angemuua kabisa. Kweli ndoa kwishinei

  ReplyDelete
 11. jamani yamekuwa hayo tena? wanaume wabaya hawa?lol

  ReplyDelete
 12. Siyo kila mwanaume ameumbwa kuwa mume, hili linajilazimisha tu kuwa mume lakini halimo kabisa. Unajua thamani ya mwanamke wewe??
  Angekuwa kaka yangu tungemkamata tumgaragaze nachukia sana wanawaume wasiojua uthamani wa mwanmke. Mwanamke kutunzwa k,kubembelezwa, mwanamke daima ni malkia kama we ni mwaume kwa nini usiende kupigana na wanaume wenzio??
  Halafu we dada utaniudhi ukiendelea kuishi na hili lidude utasikia oo ndoa kuvumilia aahhhh hakuna kitabu cha dini kilichosema ndoa ni kupigwa bibi chukua chako anza wanaume wapo maelfu ufe kwa stress na vipigo kisa kutunza ndoa??? Si dunia hii.

  ReplyDelete
 13. Dida kwa hicho kipigo na majeraha yote hayo baadaye warudiane nitamuona huyo Salha ana roho ya ajabu pia kifo chake kitakuwa mikononi mwa huyo Hammer Q.

  ReplyDelete
 14. pole sana ndugu kikubwa uzima dada angu mhhhhhhhhhhhhhh?

  ReplyDelete
 15. pole sana dada angu inaelekea broooo Hama q anawivu sana,ugua pole sister

  ReplyDelete
 16. Daah! Pole sana Salha,Mungu atakuponya jamani naona Hammer Q alitaka kuaribu reception nzuri. Hizo Bangi & Pombe lo! Mungu tunusuru na hizi ndoa zenye vipigo

  ReplyDelete
 17. HAAAAAAAAAAAAAAA HUYO DADA ALIVYO MZURI MIE NI MDADA LAKINI HUWA NAPENDA KUMUANGALIA ,LEO MWANAMME ANAMFANYIA HIVYO
  mIE NIKITOKA HAPO NOMBA TALAKA
  kABAKIA KUMUUA KWA STYLE HII
  SALHA HUYO MME HAKUFAI

  ReplyDelete
 18. pole salha hiyo sio ndoa kama anakupenda kweli asingekuumiza namna hiyo

  Mungu akunusuru mapenzi gani hayo

  ReplyDelete
 19. loo! nimechukiaje sasa!, kumbe ni yule mdada ninaependa anavyoimbaga,,
  niliposikika kwenye radio sikudhani itakuwa hivi!..huyu mume ni mbaya kweli, bora kuishi alone uwe na amani na furaha kuliko kuolewa uwe na mwenza wa dizaini hiyo, akiendelea nae anasubiri kifo tuu hapo hakuna upendo...Pole sana Salha..

  ReplyDelete
 20. Tatizo la mapenzi ya kupigana ni kuwa huyu binti akiombwa msamaha, akapewa zawadi ( sitaki kusema vizawadi) basi atarudi mambo yatakuwa mazuri kwa siku mbili yatatu wanarudia kupigana tena. Kuruhusu kupigwa ni ugonjwa mbaya sana. Mungu mnusuru huyu binti aondoke, bado ni mtoto atapata vijana wenzie.

  ReplyDelete
 21. I wish ungekuwa huku Marekani na hiyo story yako.Uwiiiiiiiiiii huyo Hammer Q angekuwa nyundo Z.Pumbavu zake.

  ReplyDelete
 22. Dida huyo mwanaume mshamba sana, kwa kua hajiamini, na wanaume wote wenye kufanyia ukatili wa namna hii wapenzi au wake zao ni washamba kabisaaaaaaaaaaaaa lol!

  ReplyDelete
 23. Hao viumbe Dida.
  Baba Zetu, Kaka Zetu, lakini jamani wengine mtihani sana.

  mmh Pole sana mamy but hapo hakuna mume. Ila sikiliza moyo wako

  ReplyDelete
 24. Hao viumbe Dida.
  Baba Zetu, Kaka Zetu, lakini jamani wengine mtihani sana.

  mmh Pole sana mamy but hapo hakuna mume. Ila sikiliza moyo wako

  ReplyDelete
 25. Pole sana dada, kaa chini utafakari hicho kipigo ndio utajua kama mumeo anakufaa au laa,utakufaa bure kisa mume mapenzi gani hayo ya kumpiga mwenzio kama mbwa mwizi!!!!!!!!!!!!! mshenzi sana huyo Hammer Q.

  ReplyDelete