MISS UTALII 2012 KAGERA

Tuesday, July 17, 2012 0 Comments

MISS UTALII KAGERA 2012 MISS IRENE BWIRE KATIKATI NA MSHINDI
WA PILI MISS JANIA ABDUL KUSHOTO NA MISS MAYOR KASHUMBA MSHINDI WATATU KULIA

Mrembo Irene bwire, mwishoni mwa wiki ameibuka mshindi wa Taji la Miss Utalii Kagera 2012, katika shindano lililo fanyika katika ukumbi wa Rinas Club mjini Bukoba mkoani kagera siku ya jumamosi tarehe
14-7-2012. Erene alitwaa taji hilo kwa kuwashinda warembo wengine 14, katika shindano ambalo mkuu wa Wilaya ya Bukoba mama Pangani alikuwa mgeni rasmi. Mrembo Jania Abdul alikuwa mshindi wa pili na Mayor
Kashumba alikuwa mshindi wa tatu, hivyo wote pamoja na mshindi wa nne,watano na mshindi wa taji la Miss Utalii Vipaji watawakilisha mkoa wa kagera katika fainali za Miss Utalii Tanzania 2012- Kanda ya
Magharibi,zitakazo fanyika mkoani Mara mwezi Oktoba 2012.


Katika shindano hilo ambalo lilisindikizwa na burudani za musiki wa asili na wa kizazi kipya wakiwemo bendi ya Diamond Sound, msanii BK Sanday  na makundi ya ngoma za asili za mkoa wa kagera,shinfano hilo
lilianndaliwa na Dinner Fashion,huku Miss Utalii Kilimanjaro 2012 Evamary Gamba akiwa ni mwalimu wa wearembo.


Mgeni raasmi , mkuu wa wilaya ya Bukoba aliwapongeza waandaaji kwa kufanikiwa kuaandaa shindano hilo ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa ni lichocheo cha kutangaza utalii na utamaduni wa mkoa wa kagera. Aidha aliema kuwa serikali na mkoa wa Kagera wanathanini sana mchango wa shindano hilo katika kuhamasisha na kutangaza utalii na utamaduni wa Tanzania pia mianya ya uwekezaji, na kuwataka wadau mbalimbali kuliunga mkono kwa kudhamini shindano hilo kla linapofanyika

0 comments: