HII NI KWA WANAWAKE WENZANGU WENYE WATOTO,MTOTO WAKO AKIFIKISHA UMRI WA MIAKA MINNE MPE MAZIWA YA NIDO NIAMINI.

Thursday, April 14, 2011 17 Comments

Katika pozi tofauti baada ya kufunga shule ni lishe kwa kwenda mbele kawa kipipa. Kameongezeka kilo mbili baada ya wiki mbili,Mpaka vitopu vinambana.
K WANZA YANAMFANYA AWE NA NGOZI NYORORO,MVUTO NA KUWA MCHANGAMFU ZAIDI NINA AMINI ILO SABABU HATA SAMIRA WANGU NAMPA NIDO TUJARIBU KUWAPA KILE AMBACHO TUNAONA KITAWASAIDIA,TUSISITE HATA KUKOSOANA NA KUSHAURIANA KWA ANAYEJUA ZAIDI KUHUSU MTOTO KWANI MTOTO WA MWENZIO NI WAKO.

17 comments:

  1. Mashallah ni kweli Samira wetu kapendeza lakini zingatia na kumfanyisha mazoezi kwakuwa siku hizi maisha yamebadilika watoto hawachezi cheza yao ni gemu kukaa na kuangalia TV kwa hiyo asije akawa mnene sana, itakuja kumletea tabu M.Mungu amnusuru kisura wetu kwani sio siri Dida Samira nampenda sana alafu Mume wangu huwaga ananambia nimefanananae kweli huniambia ukija kujaaliwa kuza utazaa watoto watakuwa wazuri kama Samira huwa na furahi sana

    ReplyDelete
  2. Dida huyu mtoto kafanana sana na mke wangu kuanzia shingo ya mkufu wa dhahabu adi jicho tafadhali usije kumvalisha bati hapo shingoni huyo ni mkewangu dhahabu kwenda mbeleee.

    ReplyDelete
  3. Dida wangu ana 5 years, anapenda nido ila anataka kulamba tu maziwa makavu hataki yafanywe chai anaweza kulamba hata kikombe kizima usipokuwa mwangalifu sijui nifanye nini, tunachofanya sasa hivi ni kuyaficha na kumdanganya kuwa yameisha, nikiwa home ndo namlazimisha anywe kama chai.. Hongera kwa mwanao looks beautiful, Mwenyezi Mungu akukuzie dada!

    ReplyDelete
  4. Samira ni km mwanangu japo simjui ila nakubaliana na maneno yako mtoto wa mwenzio ni km wako.
    Mimi ni mama wa watoto 2 maziwa ni mazuri sn sn sn kwa mtoto na hata mkubwa ila si ya unga.Nipo nje ya TZ hukuukiwa na mimba kunapewa darasa na nitabu vya kutosha kuanzia mimba mpk jinsi ya kulea mtoto mpk 5yrs.
    Maziwa fresh yanaongeza Calsium kwa mwili na kufanya mifupa ya mwili kuwa imara na kila umri wa mtoto una kilo zake kulingana na urefu wake pia ngoja nitakutumia umri na kilo yani km ana miaka 4 anapaswa kuwa na kilo flani mpk flani nitakutumia iyo kesho

    ReplyDelete
  5. Hongera Dida mimi naomba ni kukumbushe kidongo napia usisahau kumpa na matunda aina ya Apple husaidia sana kwa mtoto kutokuwa na tumbo kubwa nauzito wa kupindukia huyeyusha mafuta ya kwenye tumbo hivyo humfanya mtoto kuwa na afya nzuri huonekana mtoto mnene lakini mwenye afya kwa kuwa mafuta yasiyokuwa na lazima mwilini huondoshwa na tonda la Apple mpatie matunda mawili moja asubuhi na jengine usiku utakuwa umemsaidia sana mrembo wetu huyo M.Mungu atukuzie Amen.

    ReplyDelete
  6. Tunashukuru kwa kutupa hints za ulishaji wa watoto wetu. Hongera kwa kukuza mumy ila mi naamini kakurithi huyo maana toka naanza kukufahamu enzi za marehemu miraji upo bonge kama mwanao.

    Amanda

    ReplyDelete
  7. Mtoto anahitaji kuendelea kunywa maziwa kwa muda mrefu yaani sio akiacha kunyonya au akitimiza miaka 2 unamuachisha maziwa, hapana inabidi uendelee na maziwa ili yamsaidie kukua. Tena wakati wa kula chakula badala ya kumuwekea soda au juice unatakiwa umuwekee glasi ya maziwa. Pia uwe unampa matunda yaliyo kwenye msimu kabla hajala chakula au iwe ndio snack yake badala ya biscuits au chama. Matunda ni mazuri kwa kulinda afya ya mtoto wako bila kusahau mboga mboga za majani.

    Mpe pia yogurt au maziwa lala japo mara kwa mara ukipata yenye flavour watoto wanapenda hayo zaidi.

    Mwisho angalia asiwe overweight utaharibu afya yake ingawa wengi wanaona sifa kuwa na watoto wanene lakini obesity si nzuri waweza karibisha magonjwa hatari, maintain weight yake anayotakiwa awe nayo basi, kama yuko underweight na unataka kuongeza basi you are on the right track lakini unene si afya!

    Mwisho kabisa mpe mwanao ndizi mbivu moja kila siku kwa ajili ya ubongo wake, ndizi ni chakula cha brain utashangaa atakavyouwa anafanya vizuri shuleni!

    Ni hayo tu mdogo wangu

    Mama Dida na Iman

    ReplyDelete
  8. maziwa muhimu sana na ni mazuri kwa ngozi nywele akili na fya kwa ujumla ila mwenzangu angali hiyo nido ni oroginal maana siku hizi mhhh maziwa mengi ya kopo sio mazuri hasa hapa bongo .

    mpe ale matunda sana nakama amekuwa kipipa mpe chakula kiasi usimjazie sana na mshindilie matunda . au chukua matunda anayo ya penda umsagie kuchanganya na maziwa fresh na barafu itakuwa smooth ni nzuri sana na itamsaidie immune stystem yake!!!

    kimami

    ReplyDelete
  9. Ni kweli dida maziwa ya NIDO ni bora kwa watoto mtoto wa rafiki yangu alipokuwa na miaka mi2 alikuwa kama samira wako naye alikuwa akitumia NIDO, muongezee YOGURT na matunda kama mdau aliyetangulia alivyokushauri, nikimuona samira wako namkumbuka samira wangu alivyokuwa na umri huo alifanana sana na wako now she is 11yrs hongera dida mtunze mwanao muweke kwenye maadili ya kumtambua mwenyezi mungu ndio njia pekee itakayomuwezesha kuutambua ulimwengu Inshallah
    mama samira!

    ReplyDelete
  10. Ndio unakuwa hivyo kama huamini mtizame mwanao anavyokuwa so punguza umapepe anayaona hayo.....
    Act mama mwenye heshima zake, achana na makahaba ya mjini wengine hata watoto hawana, wameshajitoa mhanga, punguza skendo...
    Hongera kwa mwanao kuwa na afya nzuri

    ReplyDelete
  11. Mashallah,leo umenifurahisha jamani nampenda mwanao ni mie mdau niliyekuandikia nime mmiss Samira wako, asante kwa picha na hints. pia wachangiaji wengine asanteni kwa tips mlizotoa

    ReplyDelete
  12. Kumbuka kuwa kuna Childhood Obesity......

    ReplyDelete
  13. kapendeza sn samira, hd raha kweli wewe mama bora na c bora mama.nataman na mimi nzae nkimuona samira wako

    ReplyDelete
  14. Dida haka katoto karembo ulikazaa na yule mume wako wa zamani mchops? ni swali tu sio umbea..

    ReplyDelete
  15. Ni kweli. NIDO ni nzuri sana kwa watoto wanokua. Nina watoto wawili wa kiume wana afya sana na walianza kunywa NIDO tangu wakiwa na miaka 2.5, mpaka leo mmoja ana miaka 8 lakini nampa NIDO mara 1 kwa siku ila yule mdogo wa miaka 4 bado anakunya mara 2-3 kwa siku. I recommend NIDO sana, sana tu!!

    ReplyDelete
  16. Mimi nafagilia vitu fresh kwa watoto. Kwa hiyo naomba kuwashauri mumpe mtoto maziwa ya maji ya ng'ombe na si nido. Wanangu wakifika mwaka mmoja nawawekea billi ya maziwa. Hizi NIDO naziogopa sababu ya mambo ya mchina mara uansikia ooh kuna sijuhi sumu gani; ooh kuna fake. Kwa mtoto jamani tupunguze vitu vya makopo. Hata yale maziwa yaliyowapa madhara watoto wa kichina yalikuwa yamewekewa virutubisho vya kunenepesha haraka lakini bado vilikuwa ni sumu. Tuwe makini wamama wenzangu.

    ReplyDelete
  17. Hongera kwa kukuza mwanangu samira wajina wa mwanangu mashaallah ana afya njema. Ila tu usimsahau mwenyezi hivyo mtoto umpeleke madrasa hii inasaidia mtoto anakua katika maadili ya dini. Mimi naamini alivyo mrembo na akifuata maadili ya dini atapendeza zaidi pia itakuwa ni faraja hata kwako mzazi. Mimi Mama samira

    ReplyDelete