ZANTEL YAZINDUA HUDUMA YA MTANDAO NA SIMU YENYE KASI ZAIDI YA 3G /3.5G ZENJI
Kampuni ya simu inayoongoza Zanzibar na kuaminika zaidi katika
mawasiliano ya mtandao nchini, Zantel, imepiga hatua nyingine kubwa kwa
uzinduzi rasmi wa teknolojia ya mwasiliano ya 3G, ambayo itaileta huduma
ya mawasiliano ya mtandao kwa kasi ya kipekee mikononi na majumbani mwa
wazanzibar.
Teknolojia hiyo ya 3G ambayo inaenda sambamba na matarajio na uwekezaji
wa kampuni ya Zantel wenye lengo la kuifanya kampuni kuwa ya kwanza
kwenye utoaji wa huduma za mtandao na simu nchini itakuwa ya kwanza
visiwani Zanzibar.
Uzinduzi huu wa 3G utawawezezesha Wazanzibari kufurahia mawasiliano kwa
kiwango cha juu kabisa na hivyo kuwafanya kufaidi soko la biashara za
kimataifa. Kwa kutumia 3G pia, wazanzibari wataweza kuizunguka dunia na
Zanzibar kwa kasi ya ajabu.
Kasi hiyo ya ajabu itawewezesha wateja wa Zantel kuisikia sauti ya
kwanza hadi ya mwisho, huku pia wakiweza kuwapigia simu za video ndugu
zao popote duniani.
Huduma hii pia itawawezesha wazanzibari kufurahia huduma kama kutuma
picha, video, mafaili na miziki kupitia simu zao za mikononi kwa kasi
zaidi
Kiupekee zaidi huduma hii itawawezesha vijana kufurahia kutazama miziki
ikatika YOUTUBE au VIMEO kwa kasi ya pekee katika wakati huo huo kwenye
mtandao usio na kifani.
Akizungumzia huduma hizo, Afsa biashara mkuu wa Zantel Bwana Ahmed Mokhles anasema:
Akizungumzia huduma hizo, Afsa biashara mkuu wa Zantel Bwana Ahmed Mokhles anasema:
‘Uzinduzi huu unaendana sambamba na utamaduni wetu wa ugunduzi. Lakini cha msingi zaidi, tunataka kuwa wa kwanza kuwafanya Wazanzibari kuunganishwa na dunia kwa kuwaletea huduma hii ya mtandao wa kasi’
‘Hebu fikiria ni raha iliyoje kwa mwanfunzi kutoka Stone town kusoma
vitabu kupitia maktaba kubwa zaidi duniani kwa kubonyeza komputa yake
tu, au daktari wa Zanzibar kuwasiliana na wenzake duniani kote kupata
ushauri wa kidaktari au mfanyabiashara kutoka Zanzibar kuweza kununua au
kuuza kiurahisi akiwa dukani kwake’
Pamoja na uzinduzi huo wa 3G, Zantel itatoa ofa ya modemu mbili za kasi,
E 3131 na E 303 kwa bei za shilingi 30,000/- na elfu 60,000/-.
“Tutawapa wateja wetu pia aina tofauti za bunda za mtandao, ili
kuwawezesha kupata huduma watakayoimudu, lakini pia itakayoendana na
aina za maisha yao’ anasema Bwana Mokhles
Vifaa vitakavyoweza kutumia huduma hii ni pamoja na Blackberry, Iphone, Ipad na modemu za 3G. ‘3G ni teknolojia ya kipekee, lakini pia thamani inaweza kuwakilishwa
kwa binadamu katika namna ambayo inaweza kubadilisha maisha ya wateja
wetu, na mabadiliko hayo ni mengi kuyataja hapa, lakini itoshe kusema
huduma hii ya 3G itawapa nafasi Wazanzibar kujisomea, kujifunza lakini
pia kupamabana katika soko la kimataifa’.
‘Mpaka sasa, ni heshima ya pekee na jukumu la Zantel kama kampuni
inayoongoza Zanzibar kuwahakikishia Wazanzibar sio tu huduma nzuri
lakini huduma inyoweza kuwapa fursa mabalimabali kijamii na kiuchumi’
Sherehe hizi za kihistoria, ambazo zitawafanya Wazanzibari kufurahia
huduma za mtandao zilisindikizwa na Rais wa serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar, mheshimiwa Daktari Ali Mohamed Shein
0 comments: