KHADIJA KOPA AFUNIKA WASANII WA BONGOFLEVA KILI AWARDS TOUR, MOSHI.
GWIJI la Taarab nchini Tanzania kutoka kundi la TOT,
Hadija Omary Kopa na wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Ali Kiba, Omy Dimpoz, Roma
Mkatoliki AT, pamoja na wakali wa Ragge Warriors walikonga vilivyo nyoyo za
mashabiki wa burudani mjini Moshi na kudhihirisha uhalali wao wa kutwaa Tuzo
mbalimbali za Kili Music 2012.
Wasanii hao waliokuwa wakitumbuiza
katika Tamasha maalum la Kili Music Award Winners Tour lililofanyika jana
kwenye Uwanja wa Ushirika mjini hapa.
Licha ya hali ya hewa kuwa ya mvua
na manyunyu ya hapa na pale wakati wote wa tamasha hilo lakini wakazi wa mji wa
Moshi na vitongoji vyake jana walivunja rekodi ya Tamasha hilo kwa kujitokeza
kwa wingi uwanjani hapo tofauti na mikoa mingine ya Dodoma na Mwanza ambako
tayari Tanasha kama hilo limefanyika.
Kabla ya washindi wa Tuzo za Mziki
za Kilimanjaro 2012 kupanda jukwaani walianza kupandaa chipoukuzi wa tatu
wealio chuana vikali na mashabiki kumpitisha Msanii Sungura aliyeonekana
kupagawisha vilivyo kwa wimbo wake wa Ndizi
yangu.
Walianza jukwaani kupanda washindi
wa Tuzo Bora ya Wimbo wa Ragge ambayo ilitwaliwa
na kundi la Warriors from East waiotamba na vibao vyao kadhaa na kupiga
jukwaani zaidi ya saa moja na kibao cha Arusha Gold kilichopawa tuzo
kikiburudisha vilivyo na live show yao.
Mkongwe wa Taarab, Hadija Omary Kopa
aliiudhihirishia umma wa wana Kilimanjaro kuwa yeye ni Mtumbuizaji bora wa Kike
baada ya kupanda jukwaani na kuimba nyimbo zake kadhaa zilizojaa vijembe na
mashairi ya ukweli ya taarab kutoka kundi lake la TOT huku uchezaji wake
ukishangilia mwanzo hadi mwisho kwa jinsi alivyokuwa akiutikisa mwili wake.
Mkali kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi
wa Tuzo Wimbo Bora wenye Vionjo vya Kiasili AT nae alipanda jukwaani nyuma ya
Hadija Kopa na kutoa burudani ya nguvu na
wimbo wa Vifuu Utundu amabao ulimpa
tuzo aliucheza vilivyo na wanenguaji wake waili wa kike.
Akitanguliwa jukwaani na wacheza
show wake machachari alikuwa ni mshindi wa Tuzo mbili za Kili Music Award 2012,
Suma Lee aliyenyakua tuzo za wimbo bora wa Afro Pop kupiria kibao chake cha
Hakunaga na Wimbo bora wa mwaka ambao pia ni hakunaga alikamua sawasawa.
Jukwaa
lilishikwa na Omy
Dimpoz kwa kuimba nyimbo zake kadhaa ikiwapo ile iliyo mpa tuzo ya Wimbo bora
wa Kushirikishwa ya Nai Nai ambapo stejini pia alipanda Ali Kiba na
kumsindikiza live katika kibao hicho na kufumua yowe na shangwe kutoka kwa
mashabiki.
Ali Kiba alibaki jukwaani hapo na vijana
wake kumfuata kutoa shukrani zao za kupata kura zilizo wapa ushindi wa tuzo ya
Wimbo bora wa Zouk Rhumba kupitia wimbo wa Dushelele. Kiba alilimudu jukwaa
vyema kwa kucheza sambamba na vijana wake mwanzo mwisho.
Jukwaa lilichuliwa kwa muda na Mshindi
wa Tuzo ya Mwimbaji bora wa Kiume, Barnaba na kuwashukuru ndugu zake wa Moshi
kwa kumpa kura na kuwa Mchaga anaeimba vyema.
Pazia la Wasanii washindi wa tuzo za
Kili Music Award 2012 wanaofabnya ziara na waliobahatika kufika mjini Mosho
mkoani Kilimanjaro lilifungwa na Roma
Mkatoliki a.k.a Mpare wa milimani aliyeshambulia jukwaa kwa nyimbo zake kadhaa
za mistaari ya maandiko.
Roma
ambaye ni Mshindi wa tuzo mbili za Wimbo Bora wa Hip Hop kupitia wimbo wake wa
Mathematics na Tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop, alishambulia jukwaa huku
viitikio vyake vikiimbwa na DJ Choka.
Wasanii
hao wiki ijayo wanataraji kutoa burudani kama hiyo jijini Mbeya katika uwanja
wa Michezo wa Sokoine na tayari walisha tumbuiza na kuwashukuru mashabiki wao
wa Mkoani Dodoma na Jijini Mwanza.
0 comments: