KWAHERI KANUMBA, PUMZIKA KWA AMANI...

Wednesday, April 11, 2012 0 Comments


Waombolezaji wa msiba wa Marehemu Steven Charles Kanumba wakishusha jeneza lenye mwili wa marehemu  kwenye kaburi, tayari kwa kumpumuzisha katika nyumba  ya milele kwenye makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, Kanumba atakumbukwa kwa kazi yake nzuri katika tasnia ya filamu hapa nchini, ambapo alijitangaza na kuitangaza nchi vyema ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania kupitia filamu zake nyingi alizoigiza.

Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa akiuaga mwili wa mwanaye kwa mara ya mwisho kabla ya kuzikwa rasmi katika makaburi ya Kinondoni.
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa na ndugu wa karibu wakiaga mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho makaburini Kinondoni.
 Wajenzi wa kaburi la marehemu wakichanganya cementi kwa ajili ya kufukia.
 Mama wa Marehemu Steven Kanumba akiweka shada la maua kaburini
MWENZETU AMETANGULIA, AMESHAKWENDA...... 
JAPO KIROHO BADO TUPO NAE, SISI TULIOBAKI TUENDELEE KUMUENZI KWMEMA YOTE ALIYOTUACHIA, KUBWA ALILOTUHUSIA NI UPENDO
TUPENDANE
Picha zaidi tembelea Dullonet
 

0 comments: