SIMANZI KUBWA KWA TAIFA, Meli ya Abiria zaidi ya 600 imezama baharini usiku wa kuamkia leo zanzibar....!
Meli ya Spice Islander iliyokuwa ikifanya safari zake toka Unguja kuelekea Pemba ikiwa imezama ktk bahari ya Hindi, Malindi usiku wa kuamkia leo ambapo mpaka sasa inasadikika watu waliojeruhiwa wako zaidi ya 267 katika Hospital ya Mnazi mmoja Zanzibar, na maiti zaidi ya 113 zimeshapakikana na kuhifadhiwa ktk uwanja wa Maisara huku ndugu na jamaa wakizitambua
Sehemu ya umati wa watu wakiangalia kwa majonzi uokoaji ukiendelea ktk pwani hio
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein katikati akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais na Mama Mwanamwema Shein kushoto wakionekana wenye majonzi kabisa wakati walipokwenda kushuhudia majeruhi wa ajali hiyo pamoja na maiti
MUNGU AZILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO ZA WOTE WALIOFARIKI KTK AJALI HIO, NA KUWAPA NAFUU MAJERUHI WA AJALI HIO
Blog ya Mitikisiko inawapa pole ndugu na jamaa wote waliofikwa na janga hili
0 comments: