Ujio mpya wa Five Star Modern Taarab kutambulishwa Ijumaa

Monday, July 25, 2011 0 Comments

Mariam Mohamedi

Kundi la Five Stars modern taarab linatarajia kurudi upya pale litakapojitambulisha upya kwa wapenzi wa taarab na muziki kwa ujumla ktk ukumbi wa Hotel Traverntine ijumaa hii.
Bendi hio sasa itakwenda kwa jina NEW FIVE STARS MODERN TAARAB ikiwa na wasanii kibao wapya baada ya msiba mzito uliowakuta mwezi Machi mwaka huu. Baadhi ya wasanii waliojiunga na bendi hio ni pamoja na Mariam wa Bss, Musa Ally, Mafaloo Mzumbye na wengine


Utambulisho huo wa bendi utaambatana na nyimbo zao mpya ambazo zitajumuishwa ktk album yao ya kwanza ambazo ni First Lady, Sina Gubu nina sababu, watu na tabia zao, Mwenye hila habebeki na Ulaumiwe wewe nani pia utapambwa na mkali wa bongofleva Dully Sykes anayetamba na nyimbo yake ya Bongofleva.

0 comments: