TURUDI KWENYE UREMBO KIDOGO HATA USHAURI UNATOSHA.

Thursday, July 14, 2011 12 Comments

Jamani wadau hizi ni nywele zangu za kuzaliwa tatizo mbele zimekatika pls naomba ushauri kwa yoyote anayejua nizifanyaje ili mbele zijae na zisikatike?
Ahsante Reds kwa kunipa zawadi hii kunywa reds kinywaji kitamu hasa ukiwa na mwanandani wako,kinywaji safi akizeeshi kina radha taaamu sana.

12 comments:

  1. my dear hongera kumbe una nywele za kutosha, tembelea website ya Shamimu anamaadvice kibao ya kuhusu nywele kukatika etc, ila i hope katika Harusi yako utapiga weaving la nguvu.

    ReplyDelete
  2. 1.Mwone Shear wa Shear Illusion pia punguza mzigo wa maweaving kichwani zitaacha kukatika
    2. Mwone Shamim wa 8020 fashion akuuzie TT4z ni mafuta mazuri ya hair pia punguza kushonea na kujipaka migel
    3.Mashallah una uhair mrefu acha kuweka minywele bwana

    ReplyDelete
  3. Cha kwanza kabisa kwa mtazamo wangu niupunguze kuweka lace wig kwani ile gundi yake inafanya nywele laini za mbele zisikue kwa kukosa hewa na hivyo kunyonyoka au kukatika.vilevile tafuta mafuta ya TZ444 kama sikosei yamenisaidia mimi sana kurudisha nywele zangu ktk hali nzuri waweza yapata kwa shamim zeze.

    ReplyDelete
  4. Kwanza dada punguza kusuka rasta na mawiving yanakata sana nywele, kwa sasa wewe usiweke dawa zisuke tu nywele zako za kuzaliwa nazo mpaka uhakikishe zimejaa na zimeota sana, na baada ya hapo kama utaweka dawa nakushauri tumia product za olive oil, utakujaa kumbuka haya maneno imean zote olive oil cream, mafuta stearming nk. Kila kheri.

    ReplyDelete
  5. maashallah mtoto una nywele nzuri sana mie naona kwanza kabisa upunguze kuweka les wig inakukata nywele zako za mbele

    pili kama unapenda sana kulaza nywele yaani pony tail unafunga sana inachangania.

    tatu wakikuweka dawa waambiwe wasiweke na za juu hasa hapo mbele aweke tu chini na asichane kwa muda mrefu

    jitahidi usiku wakati wa kulala uweke moistaraiza alafu uzi rap vizuri na ufunge kitambaa cha satin ama kofa za kunasikia kuna mafuta yanaitwa sijui t4444 jaribu may be yatakusaidia mie sijatumia

    au ukipata ziri nyengine na ikukusaidia utuambie na sie

    kishuna

    ReplyDelete
  6. maweaving love ndo yanamaliza nywele mbele wangu zitunze tuu na ujaribu kuziacha zenyewe itakuwa sawa pole n loh mmbaya wewe hata kutualika wadau wako kwenye harusi haya hongera mwaya hehehehe hayawi hayawi leo yamekuwa alosema mtalaaka aolewi nani heheheheh DIDA juu juu daima mwaaah kisses haya waosha vinywa jimwageni uwanja nimewapa ila ukweli ndo huo dida mali ya mtu kuanzia nywele mpaka miguuu heheheehheh wakaogeeeeeee haoooooooooooo

    ReplyDelete
  7. shamimu wa 8020 ndo mtafute atakujuza. hongera dida kwa kufunga ndoa. kila la kheri mamii.

    ReplyDelete
  8. mlawa now from chiba japanJuly 19, 2011 at 2:48 PM

    mbona nzuri tu?

    ReplyDelete
  9. ahsanteni wadau wangu jamani kwa ushauri wenu nawapendaje?

    ReplyDelete
  10. HAYA TUWEKEE NA PIC ZA HARUSI YA NYWELE YASHAISHA.

    ReplyDelete
  11. Dida unaonaje ufunge blog! manake inaonekana upo bizi sana na maisha na sie tuonapenda kusoma blog yako unatukosesha raha, kila tukichungulia ni habari za mwaka arubaini na saba! ni mtazamo wangu tu.

    ReplyDelete
  12. nice hair,congrats

    ReplyDelete