JANA NIIKUWA NIMEJILAZA NIKASIKIA KENGERE INALIA GETINI,KUTAHAMAKI KUMBE KUNA MTU KAAGIZWA ANILETEE UNAVYOVIONA.

Sunday, March 13, 2011 17 Comments

Nikiwa na zawadi zangu kasheshe.
Nusu ya nyumba ni hapa mnahisi hiyo ya makumbusho niiweke wapi ni swali tu.
Walinipa na keki hii haina noma hata mie naimudu.
Tatizo hii unahisi mdau wangu niiweke wapi?

17 comments:

  1. hiyo best nahisi uweke karibu na dinning room nahisi itapendeza itafutie tu mahali pazuri pa kukaa. happy birthday dida luv u sana

    ReplyDelete
  2. hongera mpenzi, umepata zawadi nzuri kweli, yani hadi nakutamania, napenda sana vitu vya asili kama hivyo, vinaonyesha hali halisi ya maisha ya mtanzania hawa huko vijijini kwetu, da! imenikumbusha mbali sana,
    Ningekuwa mimi ndio nimepewa hiyo, ningeichongea meza yake special kabisha, nayenyewe inachongwa kiasili kidogo, then pale sitting room kwenye kona, ndio naweka hiyo nyumba juu ya meza yangu, ingekuwa mwake kweli
    hongera tena dear,

    ReplyDelete
  3. utajiju wewe mdau unayemwambia atupe huna lolote litakuivia iloooo dida kwanza big up kwako pazuri sana wewe kweli mtafutaji nakushauri itafutie meza ya kiasili kama alivyosema mdau weka hapo kwenye kona mamii itapendeza mno mwaya hongera uko juu.

    ReplyDelete
  4. Dida lazima uwe mstarabu na kupunguza kejeli kwani zawadi hata kama itakuwa pipi ni zawadi na aliekuletea ujue ana kudhamini kawapita wangapi mpaka kukupa wewe sasa kama keki wewe unaimudu basi sikia sio keki hiyo kwakuwa iyo keki umeletewa zawadi ina hadhi kuliko ndege yako mwenyewe ulio nunua kwa pesa zako inaelekea hujui maana ya zawadi.

    ReplyDelete
  5. mdau hujanielewa sikumaanisha naimudu kuinunua ninamaanisha naimudu kuila ila nimeomba kuhusu picha mnisaidie ni kitu kizuri kama cha ukumbusho nikiweke wapi sorry kama ulifikiria vibaya.Sina dharau wala kejeli basi tu mnanichukulia vingine.

    ReplyDelete
  6. kwakeli hata namie nimehisi kama dida alivyosema hata ile akili ya kusema kama dida kasema kwa ubaya sina kabisa .msiwe mnakurupuka jamani msome vizuri hivi kwani hapo kuna kitu gani hata cha kuchanganya? inaelekea wewe ni mfupi kwa mawazo na shule ilikuwa tabu kuelewa

    dida mie naona ui tengenezeee plate ya chuma ama mbao alafu uitundike sitting room tazama sehem ambyao kila mtu akiingia ataiona na kusiwe na makoro koro pembeni yake ili itulie vizuri iwish ningekuwa karibu nikutengenezee back ground yake hapo utakapo itundika

    happy beseday tu uuuuuuuu
    kishunaaa

    ReplyDelete
  7. Poa Dida nimekuwelewa nakupendeaga hapo tu uongo hutaki safi sana nimekusamehe mpenzi usijali nilikuwa sijakuelewa ulivyosema kuwa unaimudu isikonde, kuhusu picha watafute wataalamu wakujengee frem za kigae wakuzungushie alafu uiweke kwenye meza pembeni kwenye kona naamini itapendeza kwakuwa nyumba yako safi na nzuri mashaallah nizawadi nzuri sana yaani hata mimi nimeipenda icho kijiji hongera kwa kudhaminiwa.

    ReplyDelete
  8. Nashukuru kwa kunielewa ni vizuri kukosoa ahsanteni wadau.

    ReplyDelete
  9. Kwa zawadi gani babu? Itupe

    ReplyDelete
  10. kwanza hongera sana mi naona ungetafuta kameza ambako ni karefu kidogo kasiwe kafupi kawe kakiasili hivi halafu weka kwenye kakona itapendeza sana halafu nyumba yako ni nzuri sana

    ReplyDelete
  11. Wewe Anony wa 4.30pm tusitukanane bure unaposema kuwa hata shule nilikuwa mgumu kuwelewa mlete baba yako nimuone kama mfupi auala napiaa aone kama kama naelewa au la sio kuandika ili Dida akusifie nilie mwambia ni Dida na tulisha elewana sasa wewe kinakuwashia nini? unajifanya unajua kusema shauriro una mchokoza Bint wa pwani nitakuwacha hoi unijuiee nina maneno machafu kuliko karo la choo bahati yako sitaki kumkwanza mpenzi wangu dida kwakuwa nampenda sasa kwa kuwa muwazi unabahati kama ungechangia kwenye blog nyingine ungemkumbuka aliekutoa bira nanii japo umemsahau.

    ReplyDelete
  12. hamna lolote nyie waosha vinywa roho mbaya zimewazidi msokuwa na haya wala hamjui vibaya wanawake msiopenda wenzenu wapate nyooooooo dida yoyote anayekuponda jua maisha yko yanamkondesha achana nao hawana jipwa wananuka ng"onda mjini hawana lolote nguo nyeusi sabuni ya kipande midabwadaaaaaaa.tunakupenda dida ukiongea na wase.... siyo ishu fuatilia maisha yako.

    ReplyDelete
  13. hapo ndio ninapokupendea mwana huogopi kitu weka unachokitaka hujazuiliwa na utafanikiwa kwa uwezo wa manani wanakunyooshae njia wakati wenyewe wagongo kokoto chezea weye.

    ReplyDelete
  14. eeh eeh unapoweka vitu vyako open tegemea mawazo chanya na hasi dunia ndivyo ilivyo kama mnataka maoni positive tu basi wasilianeni kwenye email zenu lakini as long as different people with diffrent perspectives wanatembelea blog yako, haya hayakwepeki dada usiwe muoga.

    ReplyDelete
  15. Mambo mpendwa? hongera sana kwa kuwa na sehemu nzuri ya kuishi kwa kweli panavutia sana.kama utaona vyema naomba unisadie hili nalokuuliza, nimependa vile viatu vya kuvaa ndani ambavyo amevaa mtoto,naweza kuvipata wapi?asante kwa hilo

    ReplyDelete
  16. ningekuwa ni mimi ningetengeneza meza ambayo picha inakaa katikati ya meza, yaani, chini, miguu ya meza, inafatia mbao, then unaweka hiyo picha alafu unatengeneza kioo kwa juu, kwa hiyo mtu akiwa sebuleni amekaa kwenye kochi hivi, anaiona hiyo picha chini ya meza ya kiooo, inavutia sana hiyo picha, maana imekaa kiasili hasa, kama ujanielewa nenda pale sinza shekilango uwa wanauza fenicha meza za kioo katikati wanaweka au wanyama au ua, unaliona juu ya kioo, labda ni mtindo wa zamani, ila itapendeza, sory niko uk miaka 5 sasa sijui kama bado wako hao jamaa wa sinza....ushauri tu

    ReplyDelete