WADAU WA MUZIKI WA TAARABU,WAPENZI WA KIPINDI CHA MITIKISIKO YA PWANI KINATIMIZA MIAKA SITA.

Thursday, November 25, 2010 5 Comments

Namshukuru sana Mungu kwa kunipa pumzi na kipaji, kipindi hiki cha mitikisiko ya pwani kilianza mwaka 2004 nikiwa sijui naanzia wapi! sababu sikuwa nafahamu taarabu ni nini lkn naendelea kumshukuru TAJI LIUNDI yeye ndiye aliyegundua kipaji hiki na kulazimisha nipewe kipindi cha taarab, nilijua mjomba kanichoka maana sikujua nianzie wapi na nilikuwa sipendi kusikiliza hata hizo taarab ila namshukuru mungu na wazazi wangu walionileta duniani kiumbe mie.

Nilianza kwa shida naamini tu msemo kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha,napenda kuwashukuru wadau na wasikilizaji wa 100.5 Times fm bila nyie nisingekuwa hapa na wale ambao kwa namna moja au nyingine maneno yangu niwapo redioni yanawagusa ila ni kazi tu hupaswi kujishuku kama hujatajwa jina, jamani ni vijimambo tu.

Kutakuwa na bendi zote za taarab ikiwemo COAST MODERN, DAR MODERN, EAST AFRICAN MELOD, FIVE STAR, JAHAZI MODERN, NEW ZANZIBAR, TOT TAARAB, SUPER SHINE NA TANDALE MODERN PAMOJA NA BI KIDUDE.

Kiingilio sh 10,000 tu
Ukumbi DIAMOND JUBILEE
TAR 3 DECEMBER 2010
NYOTE TUNAWAKARIBISHA.

5 comments:

  1. pamoja sana ma tutakuja kujiachia kwa raha zetu laki si pesa chezzzzzzea mitikisiko iko juu sana hongera mdafada.

    ReplyDelete
  2. Dida,mboa unakuwa kimyaa sana jamani wenzio humu tunafungua kila siku hatukuti mambo mapya tupe raha bwana

    ReplyDelete
  3. We nawe alokwambia laki nani sasa?

    ReplyDelete
  4. hivi wewe Anonymous namba nne kwa nini unapenda kunishobokea we vipi hebu ukooooo!unataka kujulikana kupitia mina zangira heeeeee! kama una coment potezea heeeeee nakubana sana hee na bado utakereka sana mjini hapa watu wanatafuta na si kutafutana mjingamjinga wewe! kama mwanamke kweli tumia jina lako yani hadi hapo HUJIAMINI,UNANIOGOPA NA UNANIKUBALI.tehe tehe kwi kwi kwi weraaaaaa lilu lilaaaaaaaaa.

    ReplyDelete