DIAMOND MUNGU AKUJAALIE UZIDI KUFIKA MBALI KAMA IPO IPO TU MPK ULIPOFIKA UMEWAKILISHA VYEMA NCHI YETU......

Thursday, July 03, 2014 1 Comments

WASANII 12 WA TANZANIA WENYE NGUVU ZAIDI MWAKA 2014

Wana mashabiki wengi, miongoni mwao tayari ni mamilionea (wa shilingi), wapo wenye mijengo, magari ya kifahari, miradi ya biashara, makampuni, endorsements na vitu vingine. Hawa ndio wasanii 12 wa Tanzania wenye nguvu zaidi mwaka 2014.
Diamond Platnumz
10517949_331255273698429_525471304_n
Diamond Platnumz ndiye msanii anayeandikwa zaidi kwenye vyombo vya habari Afrika Mashariki kwa sasa. Hadi sasa Diamond amefikia hatua ambayo haijawahi kufikiwa na msanii yeyote wa Tanzania. Ndiye msanii mwenye show nyingi zaidi kwa sasa.
926242_1492211807681801_2068957543_n
Kimataifa 2014 umekuwa wa mafanikio zaidi kwake kuanzia kutajwa kuwania vipengele viwili kwenye tuzo za MTV MAMA, BET Awards, kushiriki kwenye wimbo uliokutanisha mastaa takriban 20 wa kampeni ya ‘Do Agric’ ‘Cocoa na Chocolate, pamoja na wimbo ‘Africa Rising’ uliomkutanisha na wasanii kama Mi Casa Music, Davido, Sarkodie na Tiwa Savage.
10251303_305719699603442_1198794320_n
Diamond akihojiwa na Karrueche Tran kwenye red carpet ya BET Awards, June 29, 2014

Pia pamoja na kufanya wimbo na Davido, Diamond ameshafanya collabo na wasanii wengine wa Nigeria wakiwemo Iyanya, Waje na Dr Sid pia hivi karibuni ameshirikishwa na kundi la Afrika Kusini, Mafikizolo.
Wema akiwa pembeni kumsupport Diamond
Diamond na Wema kwenye red carpet ya MTV MAMA 2014, Durban, SA
Pamoja na kukosa tuzo za kimataifa alizotajwa kuwania, staa huyo mwaka huu alivunja rekodi kwa kuchukua tuzo zote saba alizotajwa kwenye KTMA na pia kushinda tuzo za watu zilizotolewa June 27.
10357590_741543252534158_3703220327189885218_n
Akiwa na video mbili mpya kibindoni, moja ya wimbo aliofanya na Iyanya na ile ya wimbo wake ‘Mdogo Mdogo’, Diamond ana uhakika wa kuendelea kuutawala mwaka 2014.
Lady Jaydee
Lady Jaydee pamoja na Machozi Band akitumbuiza

1 comment:

  1. HAPO NDO WATANZANIA TUNACHELEWA . WATU WANATABASAMU MPAKA MWISHO WEWE UNAWAZA KINGEREZA CHAKE ,SIUNGEENDA WEWE

    ReplyDelete