MAHABA USINITOE DAMU KUDADEKIIII...
Shilole azungumzia uamuzi wa Nuh Mziwanda kujichora Tattoo ya jina lake isiyofutika
Mwanzoni mwa wiki hii, Nuh Mziwanda ambaye ni mpenzi wa
Shilole aka ShiShi Baby alijichora tattoo ya kudumu yenye jina la
Shilole.
Akiongea na The Jump Off ya 100.5 Times Fm, Nuh Mziwanda alieleza
kuwa tattoo aliyochora ni ya kudumu na kwamba atakufa akiwa na tattoo
hiyo.
Aliongeza kuwa hata kama Shilole atakuja kumuacha yeye hajali
kitakachotokea anachojali ni kuwa anampenda na ameyabadilisha maisha
yake kwa upekee wake.
Tuliongea na Shilole kuhusu uamuzi wa Nuh Mziwanda na jinsi anavyouchukulia.
“Hata sijui nisemeje…unajua kuchora kitu kwenye mwili ambacho sio cha
kwako ni ngumu sana. Kwa hiyo yeye uamuzi wake aliouchukua,
hakulazimishwa na mtu alifanya mwenyewe kwa mapenzi. Kwa hiyo aliamua
kwa kuwa analove na mimi na ninalove na yeye basi ndio maana akaamua
kufanya vile. Mimi kwangu ina maana kubwa sana sio siri ambayo
haielezeki.
Tulitaka kufamu kama Shilole na yeye ana mpango wa kuja kuchora tattoo yenye jina la Nuh Mziwanda.
“Hamna…siwezi kusema ntafanya hivyo sijui na nini basi ni mapenzi
tu na mimi siku nikiamua kufanya ntafanya kama ambavyo amefanya yeye.
Kiukweli ana love ya ukweli kabisa tofauti na wanaume ambao nilikuwa
nao, watu walikuwa wanapenda tu wasikie wanatoka na ShiShi kwa kutaka
kutafuta ‘kick’ na nini…lakini Nu h kama Nuh ana upendo wa peke yake
kabisa. Yaani hadi inafikia hatua nasema alikuwa wapi. Wanasema Mungu
akitaka kukupa kitu hakuandikii barua.”
.png)







0 comments: