HAYA HAYA TENA MAPENZI YA FACEBOOK KUDADADEKI SUBIRINI TU KAMA IPO IPO TU SUBIRI KAMA UKO KWENYE FOLENI YA KIKOMBE CHA BABU LOLIONDO,KAMA IPO IPO TU ....

Wednesday, June 11, 2014 1 Comments

Mwanaume mmoja nchini Morocco anashikiliwa na polisi baada ya kumzika hai mpenzi wake ambaye walifahamina kupitia internet.

Baada ya mawasiliano na mazungumzo ya kimapenzi kunoga kupitia mtandao binti wa miaka 25 kutoka Ufaransa Mina El Houari alisafiri mpaka Morocco kuonana na mpenzi wake huyo ambaye hawafahamina kwa sura lakini alipofika katika mji wa Fez alianza kujisikia anaumwa sana.

Bila kujua binti huyo ana kisukari mwanaume huyo anasema alimuona Mina akianguka huku akiwa na hali mbaya na kwa madai yake akafikiri amekufa kwa hiyo akamzika!

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi,Mina alikuwa bado mzima ila alikuwa ana hali mbaya na aliaga dunia baada ya kufunikwa na udongo yaani kuzikwa hai.

Haya tabia ya mabinti kuanzisha uhusiano na wanaume msiowajua huko kwenye mitandao mmeona yaliyomkuta mwenzenu?

1 comment: