WAZEE NDIO WALIWEZA KUDUMU KIZAZI CHA SASA NI SHIDA....

Friday, December 20, 2013 5 Comments

BOB JUNIOR: Kuwa bachelor raha...sioi tena ngó!!

Mwimbaji na mtayarishaji wa muziki Bob Junior au Sharobaro President amesema kuwa hana mpango wa kuoa tena baada ya kuachana na mkewe.
Sharobaro President ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa kutokana na kusumbuliwa na ndoa yake na kukosa furaha katika maisha ya ndoa, ameamua kuachana na habari za kuoa na kuishi ki-bachelor kwa kuwa ameona shida ya ndoa na raha ya kuishi kibachelor.

“I’m single, sitaoa tena…mimi niko single na sitaoa tena. Kwa sababu nimeona ugumu wa ndoa na wepesi wa kuwa bachelor. Kwa hiyo nimeamua kuwa bachelor na siwezi kuoa tena, sioi tena jamani I’m single. No more kuoa Bob Junior” Bob Junior ameiambia tovuti ya Times Fm.

“Unajua unapokuwa kwenye mahusiano ya boyfriend na girlfriend, hamna ile ‘uko wapi sasa hivi, rudi haraka nyumbani’, umeenda kwenye show ukirudi mara kanuna.”

Ameeleza kuwa ndoa yake ilikuwa inarudisha nyuma maendeleo ya  kazi yake kwa kuwa katika siku saba za wiki ni siku mbili tu anakuwa na furaha, na kwa kuwa kazi yake inategemea ubunifu na utulivu asingeweza kufanya kazi vizuri.

Amesema mkewe alikuwa na wivu na alikuwa akiingilia hadi ukurasa wake wa facebook na kuwatukana watu waliokuwa wanachat nae.

Katika hatua nyingine, Bob Junior ameelezea kuhusu kufuatiliwa mara kwa mara na baadhi ya magazeti na kumuandika vibaya, ambapo amesema ukubwa wa jina lake ndio chanzo cha kuandikwa.Amesema amejaribu kuwakataza lakini anaona wanaendelea.

Kuhusu kuandikwa kuwa ni Freemason katika kipindi cha hivi karibuni, alifunguka:
“Kuna picha ambayo niliweka alama ya Freemason. Kwa hiyo kila nikijaribu kuwakatalia nashindwa kwa sababu picha inaonesha ushahidi kwamba mimi niko kwenye hiyo dini, wakati ukweli mimi siko katika dini hiyo. Kwa hiyo kila siku wanajaribu kutafuta vitu vipya. So nadhani ni wakati wangu tu ndio maana wanajaribu kuandika hivyo.”

Usikose kusikiliza kipindi cha The Jump Off ya 100.5 Times Fm, na Bongo Dot Home wiki hii kwa undani zaidi wa story hii.
Habari kwa hisani ya tovuti ya Times fm.

5 comments:

 1. NYUMBA MAKUTI TENA YA KUUNGA UNGA BOB.MKE YAKE MATUNZO.
  MIE NILIOLEWA MDOGO NA NIKAACHA YOTE YA UJANA MNA MUME AKAACHA TUMEISHI ,SASA UOWE NA BADO UKO FACEBOOK MUDA MWINGI UNADANI NINI KITATOKEA SKENDO KIBAO.
  MKEO ALIFANYA MAKOSA KUKUZALIA MAPEMA ANGEKUSOMA KWANZA KWANI ALIJUA WEWE NI SHAROBARO NA PESA INAINGIA NA MZIKI ,SIJUI KWANINI ALIAMUA KUZAA.MNA MTESA MTOTO ANAKOSA MAPENZ YA WAZAZI
  VIJANA FIKIRIENI KABLA

  ReplyDelete
 2. DIDA TUPE RATIBA YA VIPINDI SIE WA SWEDEN PLEAS

  ReplyDelete
  Replies
  1. na mimi ni mtanzania nipo sweden je wewe uko sweden mji gani?

   Delete
 3. ushaachika tena nini?mbona maneno shosti

  ReplyDelete
 4. Hovyo.....Mwenyewe unaona siiifa! Hao wanaokusema uko Freemason wala hawawajui Freemason ni kina nani. Wewe huwezi kuwa Freemason! Kwendraaaaaaa

  ReplyDelete