TUACHE KUMSINGIZIA SHETANI WAKATI MWINGINE
Msanii wa Kenya mwenye
wimbo wa “Sina Beef” aitwae Maleek amefanya kitendo cha kusikitisha sana baada
ya kutangaza motto wake amefariki na kuomba michango hali halisi ikiwa motto
wake mzima kabisa.
Ilivyoanza msanii huyo
ali-post katika ukurasa wake wa facebook kua Binti yake mgonjwa sana, na baada
ya siku mbili aka-post tena kua binti yake amefariki tena kwa quote na mistari
ya Biblia kila baada ya muda mfupi akionyesha ni jinsi gani ameguswa na msiba
huo (Feki).
MALEEK
Wa-kenya wenzie wakawa
wamemchangia pesa na walipokwenda nyumbani kwake ili kushiriki nae msiba
walishangazwa kumkuta marehemu akicheza kama kawaida na katika njema kabisa.
Watu wakapandwa hasira
sana baada ya kugundua mchezo mzima wampigia simu ambapo akawa hapatikani baada
ya muda wakampata kwa simu na kuanza kuwaomba msamaha akidai kua ni SHETANI TU
ALIMPITIA na akawaahidi kua atarudisha pesa zote ambazo ni zaidi ya LAKI 3 za
Kenya.
Huyo angepelekwa kwa pilato! Angekua hana pesa ye angeomba tu ilo ni jibwa
ReplyDelete