TUZO ZA KTMA 2013 ZILIVYOKUA J’MOSI...

Monday, June 10, 2013 0 Comments

HATIMAYE kitendawili cha nani kavuna nini katika kinyang’anyiro Kilimanjaro Tanzania Music Awards KTMA 2013, kilipata jibu usiku wa jumamosi, ambapo kategori zote za mchakato huo zilipata washindi, huku wasanii Kala Jeremiah na Ommy Dimpoz wakifunika kwa upande wa muziki wa kizazi kipya.



 
Kala Jeremiah akimaliza kwa kutwaa tuzo tatu za Wimbo Bora wa Mwaka (Dear God), Msanii Bora wa Hip Hop na ile ya Mtunzi Bora Bora wa Hip Hop, huku akiipoteza ya Wimbo Bora wa Mwaka wa Hip Hop(Dear God) iliyochukuliwa na Nay wa Mitego kuptia wimbo Nasema Nao.



 
Kwa upande wa Dimpoz, nyota pekee aliyekuwa akiwania tuzo saba katika kinyang’anyiro hicho, alipata tuzo tatu za Wimbo Bora wa Bongo Pop (Me and You feat Vanessa Mdee), kibao kilichompa pia tuzo ya Wimbo Bora wa Ushirikiano.



 
Dimpoz akapokea tuzo ya tatu ya Video Bora ya Mwaka kupitia kibao cha Baadae,huku akiangukia pua katika kategori nne za Wimbo Bora wa Mwaka, Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume, Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume – Bongo Flava na Mtunzi Bora wa Mashairi – Bongo Flava.
 
Katika namna iliyowavutia wengi, Dimpoz aliitoa kwa Vanessa Mdee moja ya tuzo mbili alizoshinda kupitia kibao alichomshirikisha cha Me and You kwa, tukio lililotafsiriwa kama ‘kumpoza’ binti huyo aliyeangukia pua katika kategori ya Msanii Bora Anayechipukia, ambayo ilienda kwa Ali Nipishe.



 
Bendi ya Mashujaa waliibuka kidedea zaidi katika mchakato huo, baada ya kujizolea tuzo tano, kupitia mbili za bendi (Wimbo Bora wa Bendi – Risasi Kidole) na Bendi Bora ya Mwaka, huku ikitwaa tatu za wasanii wake, ambao ni Chalz Baba aliyetwaa mbili za Mtunzi Bora wa Mashairi – Bendi na Msanii Bora wa Kiume – Bendi.
 
Pia rapa wake Ferguson aliibuka kidedea katika kategori ya Rappa Bora wa Bendi, alikowabwaga Greyson Semsekwa, J4, Jonico Flower na Sauti ya Radi.
 
Ukiondoa washindi wa Kategori 35, KTMA 2013 ilitoa tuzo mbili maalum; moja ya All of Fame ilitwaliwa na kundi la Kilimanjaro Band ‘Wana Njenje’ ambayo ilipokelewa na Waziri Ali, huku ile ya Individual All of Fame ikinyakuliwa na nyota wa muziki wa zamani marehemu Salum Abdallah na kupokelewa na mwanaye.
 


0 comments: