HONGERA REHEMA KILUVIA KWA KITCHEN PARTY YAKO BIBI,MUNGU AKUJAALIE NDOA IPITE SALAMA BOFYA UJIONEE MAMBO.
Rehema katika vazi la pili,mtoto baby face kwa raha zake akijifaragua.
Shurti jiugongwa la shamim zeze bibi.
Muonekano wa ukumbi .
Dada wa bibi harusi anaitwa mamaa Lulu kiluvia akikumbatiana muda mfupi baada ya kumkabidhi gari aina ya FUN CARGO mambo ya mutoto wa mujini mamaa luluuu wakuache.
Wakicheza kwa raha zao.
Mc akifanya vitu vyake.
Awamu ya kwanza mtoto alitoka na vazi ilo mnaloliona.
Wacha we MRS G Mwanamke kimino.
Twanga pepeta ndani Bi harusi ni mpenzi sana wa twanga hawakuwa na budi kuja kumpongeza full kujiachia na shoo ya maana.
Hayo ni baadhi yaliyojiri tunakutakia kila lakheri rehema ndoa tamuuuuuuuuuu anayesema shubiri mbona yeye kaganda kama ruba ndani ahatokiiiiii.
Sema staghafirullah Dida wewe mungu akunusuru yasije kukukuta unafikiri watu wanapenda kuachana, mfano mzuri kwako unaweza kutueleza kilichokukimbiza kwa Mchops?
ReplyDeleteUliwahi kufanyiwa singo wewe la sahani, kibakuli na kikombe cha chai chenye kisosi? Humu unafundishwa tamu na chungu ya ndoa, kama hukuipata mwambie somo yako akufanyie.
Nakuapia ukiipa hiyo, hutaondoka kwa mume hata kama anakunyanyasa maana ukiikumbuka hiyo siku na maneno uliyokuwa ukielezwa utaishia kulia tu na hutamwambia yeyote kwa kukwepa aibu ndugu yangu.
Nakupenda ndugu yangu wala sikuchukii ndio mana nina kwambia haya.
aminia mama kiluvia pendeza sana !!!!!funga midomo
ReplyDeleteHata kama chungu watu wanavumilia na alivyosema dida ni sawa ndoa bwana ina ugumu wake lakini maisha ya ndoa ya huyu kamwe hayafanani na ya yule na hatuwezi kumwambia be harusi itakuwa hivi na hivi mana maisha anayoenda kuishi yeye na mumewe ni mapya huwezi kuyalinganisha na ya wengine mana hakuna aliyewai kuyaishi wao ndo wanaenda kuyaanza yatakuwaje we will never know.
ReplyDelete