UHALIFU MPYA- KAA CHONJO

Monday, January 30, 2012 1 Comments


KUMEZUKA WIMBI JIPYA LA UHALIFU, HII IKO NAMNA HII:-

UNAKUTA MFUKO WA NYLON( MAARUFU KAMA MIFUKO YA CONDOM,RAMBO,PLASTIC)
BARABARANI . UKIUKANYAGA TU LAZIMA UTAPATA PUNCHER MAANA NDANI YAKE
KUNA KIBAO KILICHOPIGILIWA MISUMARI ZAIDI YA UNAVYOFIKIRIA WEWE.
UKISHUKA GARINI KUANGALIA KULIKONI WIMBI LA VIBAKA LINAKUVAMIA NA
HAKUNA UTAKACHOBAKIA NACHO ZAIDI YA GARI MAANA LITAKUWA HALINA UPEPO
BAADHI YA MAGURUDUMU.VIBAO NI VINGI KWA UMBALI MFUPI MFUPI.HII
IMETOKEA JANA TABATA KISUKURU MAENEO YA MAKOKA MIDA YA SAA TATU USIKU.
WALIOPATA PUNCHER NI PAMOJA NA MKE WANGU NA MAGARI MENGINE KIBAO,
WALIOLIFANIKIWA KUIBIWA SIJAPATA TAARIFA BADO ILA TULIJI-ORGANISE NA
KUPITA NJIA ZOTE NA KUVUKUSANYA.



WATAKUPIGA KIASI GANI HIYO INATEGEMEA KIWANGO CHA BANGI WALICHOVUTA NA
UNAJEURI KIASI GANI.



TAHADHARI.

USIKANYAGE MFUKO WA NYLON ( KWEPA).

UKIKANYAGA BAHATI MBAYA JIANDAE VYEMA KABLA YA KUSHUKA GARINI AU
TEMBEA NA PUNCHER UMBALI KIDOGO.



MTAARIFU NA MWENZAKO.

Kwa Hisani ya Mdau

1 comment:

  1. HAPO BANGI IMEKOSA NINI? TUELIMIKE JAMANI, NI MMEA UMEUBWA KAMA ULIVYOUMBWA MCHICHA, NI AKILI ZA WATU WASIOTAKA MAENDELEO, LAKINI TUSISINGIZIE BANGI

    ReplyDelete