LEO NDIO LEO APATAE UJEMBE AMPE NA MWENZIE.

Friday, January 07, 2011 7 Comments

Huwa tunazungumza mambo mengi sana akheri ya mchawi kuliko mmbea,huu ni mwaka mwengine mbinu mbali mbali zimewekwa kwa ajili ya wale wapenda kuyazungumza ya watu ya kwake kayawekea mito anayalalia,Sasa ni wakati wa kufanya maendeleo zaidi kwa nini uwe na roho mbaya mpaka ufike kumuharibia mtu maisha na hata kwenye mahusiano ya wenzio inahuuu,Fanya maisha yako usitake yawenzio hayakuhusuu na mtababuka mwaka huu,
Mfano kumuharibia mwenzio kwa mpenzi wake ni vipi hapo atakuoa wewe?au utamuoa wewe? na kwenye kazi kumpikia mwenzio majungu haonekane hafai mshahara wake utalipwa wewe? acheni hizo kila siku ni majungu mnapata faida gani embu badilikeni mkisutwa kwa matarumbeta utasema wenzio waswahili acheni roho za karatasi mkilowa hamna maaana likikugusa waweza bofya kwengine hapa ni wakati wa kupeana joto ukipata harara tumia protex.

7 comments:

  1. hahahha dida yani we kiboko wa mipasho waambiye hao wenye roho za karatasiiiiiiii halo haloooo tena roho zako makaratasi yale nyyaaaa hahahha dida tunakumind ile mbaya huku ndugu yangu usichoke waambiye mie tu maneno yako yani yannikosha kwelikweli hahhah kuna joto wakipata harara watumie protex hahahahhahhah

    ila shosti bana uwe mwepesi kutufanyia update bana aah tunakuja chungulia kila siku pako holaaa

    ReplyDelete
  2. hahaha watajuta kukufahamu dida maneno yako huwa ni mkuki jamani unanifariji na kama huyo anon alivyosema tunahitaji sana vijembe vyako kuna watu vinawachoma usiwe unakaa kimya bwana tunamiss mambo nakupenda wewe dida acha tu kazi tu majungu kwao

    ReplyDelete
  3. Kweli mwaka umeanza ulipotelea wapi wewe kitukuu cha wamanyema, ukichanganya na Tanga ooh rahaa. Maneno ya leo ningekuwa karibu ningekununulia Mirinda baridii upooze koo lol! Tena wengine hawana haya wala hawajui vibaya, hivi mtu ukamfanyie majungu dada yako au wifi yako inahuu? Huyo mume akimuacha atakuoa wewe au atakuja kumuoa mkeo? Haloo!

    Na tena mbali na majungu mtu unaungulika dada yako akipata inahuu, yani wewe kila siku nduguzo wakuzaliwa nao tumbo moja huwasaidii ndewe wala sikio wamejihangakia wenyewe maisha yamekubali roho inakuuma, ulitaka kila siku wawe wankulilia shida? Na hata walipokuwa na shida msaada wako elfu 20 na matangazo na masimango juu! Leo hawakuombi senti roho inakuuma, majungu, fitna na roho ya karatasi tena karatasi lenyewe toilet paper. Dida leo umenifanya nitoe mfundo wangu, mwenyewe akisoma anajijua lakini si tunamwambia Mlango wa Mungu Uwazi hata afanyeje yeye ndiye mtoa riziki!

    ReplyDelete
  4. yaaani hii ni kweli kabisa yaaani hili neno...!!!

    ReplyDelete
  5. yeaaaaaaah nimefurahisana ujumbe umewafikia wachonga ngenga wapewape mamito,watanyooka tu mmoja baada ya mmoja maneno mbukwa hayo.




    Amina Zangira

    ReplyDelete
  6. tena kwa maoffisini kuna makabila flani flani wao umbea ni jadi yao mpaka wakapata jina la mkoa majungu fitna uchawi harafuu wanajifanya walokole chezea mungu eeenh

    wape dida penda sana hiii
    OddoIddi

    ReplyDelete
  7. yaani dida hili waanzie nalomwaka.tabia hii itawakoseshea madili ya maana na watu wa maana.halafu wao wanajisahau kujiongeleana kujiangalia mwisho wa kishtuka wako nyumaaaaa basi wanaanza tena majungu oo wale wanajifanya wanapesa ooh wanajidai wanajisikia!!wenzenu wana focus.poleni...stockholm...

    ReplyDelete