KARIBU HOME...

Friday, July 11, 2014 0 Comments

MAPOKEZI YA DIAMOND PLATNUMZ AKITOKEA MAREKANI KATIKA TUZO ZA BET

Tarehe 10/7/2014 ni siku ambayo Star wa muziki wa Bongo fleva nchini Tanzania Diamond Platnumz, ambaye anachafua anga la muziki kwa sasa kwa utunzi na uimbaji wake alitua katika Uwanja wa Ndege Mwal. Jurius Nyerere, mnamo mishare ya saa nne na nusu za usiku akitokea nchini Marekani ambapo alikua huko kushiriki katika Tuzo kubwa Dunia  BET awards, ambazo hufanyika kila mwaka, Diamond alikua katika kategori ya Best African Act ambayo ilichukuliwa na Davido kutoka Nigeria.........
Watanzania wenye moyo wa Upendo na Kizalendo walijitokeza katika viwanja vya ndege kumpokea Msanii huyo, wakiwa na mabango makubwa kabisa yenye maneno ya kuashiria ushujaa aliouonyesha Diamond katika muziki na kuipeperusha vyema  Bendera ya Tanzania katika muziki, Uwanja wa ndege wa Mwl. Julius Nyerere, uligubikwa na Kelele za Furaha na Sauti zilisikika zikiimba wimbo wa Mdogomdogo ikiwa ni mapenzi ya dhati kabisa kwa Diamond kwa kutuwakilisha vema na kurejea salama, hakika kazi ya muziki wetu kwa sasa inaonekana..........

0 comments: