Times Fm yachangia chama cha Albino Temeke shilingi milioni tatu...
100.5 Times Fm Radio imetoa kiasi cha shilingi milioni tatu
kwa albino wa wilaya ya Temeke, Dar es Salaam kama sehemu ya mchango wao
kwa jamii hiyo yenye ulemavu wa ngozi inayokumbwa na changamoto nyingi.
Katibu wa Kampuni ya Times Fm Radio, Amani Joachim ameukabidhi
uongozi wa chama hicho hundi halisi akiwa ameambatana na Aluta Warioba
(Meneja Vipindi Msaidizi) na Mzee Chapuo kutoka katika idara ya ubunifu.
Amani Joachim aliwaomba wapokee kiasi hicho kwa kuwa bado Times Fm
itaendelea kushirikiana nao katika kupambana na changamoto
zinazowakabili na kuhamasisha jamii kuendelea kuonesha upendo kwa
walemavu.
Baada ya kupokea hundi halisi ya kiasi hicho cha fedha, mwenyekiti wa
chama cha Albino Temeke, Khasim Kibwe alitoa shukurani zake kwa chombo
hicho cha radio na kueleza kuwa fedha hizo zitasaidia sana katika
kununua mafuta maalum ya ngozi kwa wanachama wake.
“Kwanza nafurahi sana kwa kutujali sisi Albino. Lakini vilevile wito
kwa jamii nao waige mfano huu wa 100.5 Times Fm nao waweze kuwachangia
watu wenye albinism. Baada ya kuwa kiongozi, nakumbuka hata
mlipotushirikisha katika mpira mwaka 2008 tuliona urafiki wenu wa
karibu, vilevile sasa tunauona urafiki wenu umekamilika zaidi. Ni watu
ambao mnajali watu wenye mahitaji maalum.
“Jamii iendelee kusikiliza Times Fm na wale wenye mahitaji wengine
basi waipende Times kwa kuwa inapenda watu wa aina zote.” Amesema bwana
Kibwe.
Viongozi wengine wa chama hicho waliokuwepo ni pamoja na muweka hazina, Said Ndonge na katibu wa chama, Gaston Mcheka.
.png)







0 comments: