MUNGU MKUBWA....

Monday, June 30, 2014 0 Comments

Mgonjwa wa kansa afunga ndoa hospitali na mwanamke anayempenda na kufariki masaa 10 mbele


Katika hali ya kusikitisha,kijana mdogo mwenye miaka 29 aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa aliamua kufunga ndoa na mpenzi wake hospitali (Philippines hospital) na masaa 10 mbele akafariki dunia.

Kabla hajalazwa hospitali hapo May Rowden Go Pangcoga aliyekuwa akisumbuliwa na kansa ya ini ambayo ilifikia hatua ya nne alikuwa na ndoto ya kumuoa mama wa mtoto na mpenzi wake aliyempenda sana Leizl na ndoa ilipangwa ifanyike mwezi July.

Kaka yake aitwae Hasset alituma video akisema ndugu yake hakuweza kutoka hospitali ili kutimiza alichokusudia na badala yake wakamletea kanisa hospitali na baada ya masaa 10 ya kusherekea ndoa yao na marafiki na ndugu Rowden alipoteza maisha yake kwa ugonjwa wa kansa!

Cheki picha ya tukio kamili lilivyokuwa.

0 comments: