NIMEANZA KUJIFUA MPAKA KIELEWEKE

Wednesday, May 15, 2013 11 Comments

Nikikaa kwa muda mrefu bila zoezi naona nanenepa sana, na round hii nimeanza mazoezi ya kufa mtu, full gym yaani mpaka kieleweke. Leeo katika mazoezi yangu nimekutana na wapenda mazoezi wengine Ray (Actor Bongo Movie) Pamoja na Odama (Actress Bongo Movie)
Kupumzika muhimu, na mazoezi kwa hatua, si mchezo.

Hapa baada ya mazoezi actor and Actress RAY na ODAMA wa Bongo Movie. Kweli ukipiga tizi unapungua, Ray ,ameweza ku-lose weight hadi kitambi hakionekani. Star wa Movie nna mazoezi jamani You have to stay in shape. 
Sio kwenye movie ukiambiwa hata kukimbia inakua taabu

Na mazoezi jamani yanatuweka mbali na kuugua ugua magonjwa mbalimbali

Na huu ndio muonekano mpya wa Actor RAY (Bongo Movie) kwasasa baada ya kupiga mazoezi kwa sana.
KWA HIYO NDUGU ZANGU TUSIJISAHAU MAZOEZI MUHIMU SANA HATA KIAFYA PIA.

11 comments:

  1. Ni bora sana Dida kama utapungua ili ubadilishe muonekano, nahisi utakua mrembo zaidi.

    ReplyDelete
  2. Kwa mimi Dida nilikuwa na kilo 89 na ufupi kama wewe,nilianza gym miez miwili nilipungua tukilo tuwili tu,tena pale oil com sayansi,nikaona ujinga mtu akanishauri gym ni kwa ajili ya kumaintain weight yako tu na upunguz calories nying coz ya mashine,jaribu kwenda uwanjani shule za kayumba jion au asubuhi siku za weekend kimbia pale na fanya diet ya one week nilipungu 3kg

    ReplyDelete
  3. Sio kufanya mazoezi tu, unatakiwa upunguze na kula pia. Yaani ule chakula kiasi, sio lazima ushibe mpaka ushindwe kunyanyuka, itakuwa kazi bure. Maana ukishapiga zoezi njaa ile mbaya, ndio maana akina power mabula wanafanya mazoezi sana lakini wanakula ugali kilo 3 nyama kilo 6 ktk mlo mmoja.

    ReplyDelete
  4. kaza buti mamaa.. mazoezi siku zote yanahitaji discipline. Na pia discipline ya kula. Badala ya kula chipsi mara mbili kwa siku kula once and nyingine kunywa fluids (sio soda but maji or juice) kufidia chipsi ambazo ungekula. Unaweza kupungua fasta mwanzoni afu inafika kipindi unakuwa upo still hupungui, usiache mazoezi endelea n stick na diet yako nzuri n utaona tu mafanikio. Kuna msemo unasema: wewe ni unachokula!! so bonge lazima kuna milo flani anafakamia n mwembamba kula discipline flani anayo kwenye mambo ya kula. Kila la kheri

    Halafu Dida, please tafadhali hio playlist ya humu ulioiweka naomba mwambie mtu wako wa website aifanye iwe option, anaetaka kuskiliza ndo askilize, isiwe lazima kwamba ukifungua page tu miziki inaanza. Mwisho inakuwa karaha badala ya raha.

    ReplyDelete
  5. HAYA HAYA HARAKA MKATAFUTE RABA ZA MAZOEZI WOTE 3

    ReplyDelete
  6. ray kapungua sana,alikuwa na kitambi hicho,chote kimeisha.na wewe dida hivyo viatu sio vya kufanyia mazoezi,nyayo zote si zitakuuma?

    ReplyDelete
    Replies
    1. mtajibebah@muke ya masaiMay 16, 2013 at 12:44 PM

      ray upunguaji wake kanywa madawa kwanza ndo maana kapuputika namna hiyo ungekuwa upunguaji wa diet tu na mazoezi wala asingekuwa hivo ghafla nyiee...,upunguaji wa madawa unakuwa kama yeye kama mtu mgonjwa na alikunywa nyingi angekunywa kidogo angejiona yuko poa kidogo tu angeziacha nakisha na kuendelea kujinyima kula angekuwa poa sana ......sasa hapo inabidi ajiweke sawa awe kidogo mwenye kuvutia

      Delete
  7. Mm naona ubaki tu na mwili wako ila umantain usizid!dida sura yako imejaa!ht ukipungua sura bado haipungui!kwa hyo ukipungua uso utakuwa hauendani na mwili!we mwenyewe hujion kwenye michezo yako ya kaole?ule mwili ulokuwa nao haukuwa unakupendeza!ulikuwa unakuonesha sura kubwa mwili mdogo!ila hvyo ulivyo sasa ndo vimeendana!sura na mwili uwiano sawa kabisa!jimantain na upunguze tumbo tu!ckushaur ujikondeshe!kuna miili inayopendeza wakipungua ila si wewe mpendwa.

    ReplyDelete
  8. didaa mi nataka kujua hz trouser au tight naweza kuzipata dukani kwako?hz za mazoezi au mwny kujua ntazipata wapi msaada wa haraka unahitajikaaa

    ReplyDelete
  9. Hapo umenifurahisha Dida kwa kuanza maxoezi, safi sana ila usichoke, ukipungua nitakupenda zaidi....

    ReplyDelete