UHARAMIA WA KAZI ZA WASANII KUKOMESHWA

Tuesday, May 22, 2012 1 Comments

Mtendaji kutoka Kampuni ya Global StandardOne (GS1), Andrew Karumuna akionesha moja ya kazi ya Msanii Judith Wambura(Lady Jay Dee) iliyowekewa alama maalum ya kimataifa ya utambuzi na udhibiti wabidhaa kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii.Lady Jay Dee ni msanii pekee ambayeamekwishaingia na kuanza kunufaika na mfumo huu.

 
 Bi. Fatma Kange akiongea na wadau wa Sanaakuhusu mfumo maalum wa kimataifa wa utambuzi na udhibiti wa bidhaa mbalimbaliwakati akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari, BASATA GodfreyLebejo na Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego. 


Na Aristide Kwizela, BASATA
Huenda kilio cha wasaniijuu ya wizi wa kazi zao kikapungua kama si kufikia kikomo iwapo wasaniiwataamka na kushirikiana na kampuni ya Global Standard One (GS1) ambayo imekujana mfumo wa kimataifa wa kutambua na kudhibiti kazi za Sanaa.

Akizungumza wiki hii kwenyeJukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kaimu Mkurugenzi wa kampuni hiyo Fatma Kange alisema kuwa, mfumo huo wa kuziwekea alama ya utambuzi yakimataifa (barcode) kazi za wasanii utasaidia kudhibiti uharamia kwenye sektaya sanaa na kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi.

“Mfumo huu ni wa kimataifa,umekuwa ukitumika duniani kote miaka 38 iliyopita, hapa kwetu ni mpya kabisa.Ni mfumo wa kutambua bidhaa halali kwa kuziwekea alama maalum (barcode) ambayoitazifanya zitambuliwe kimataifa na kutokughushiwa” alisema Bi. Kange.

 Aliongeza kuwa, mfumo huounalenga kurasimisha sekta ya Sanaa kwa kuwafanya wasanii kwanza kujisajili nabaadaye kazi zao kuwekewa alama maalum ambapo sasa watajua idadi halisi ya nakala(bidhaa za sanaa) walizozalisha, fedha walizoingiza na zaidi kutazuia kazi zaokuuzwa hovyo mitaani pasipokufuata taratibu.

“Lengo ni kazi za wasanii kutambuliwa kimataifa, kuuzwa kwenye maduka makubwa na kupewa thamani halisi.Wenzetu katika nchi zilizoendelea wako mbali katika hili, kazi zao zinauzwakwenye art stores tu (maduka maalum ya kazi za Sanaa)” alisisitiza Kange.

Akieleza jinsi Wasanii watakavyojiunga, Bi. Kange alisema kuwa, wako kwenye mikakati ya kuwaelimishaWasanii lakini akasisitiza kuwa, mfumo huo huendeshwa kwa wasanii wenyewekuridhia na baadaye kazi zao kuwekewa alama hiyo ambapo hukatwa kiwango kidogosana cha fedha baada ya kukubaliana na wasanii wote.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego alisema kuwa, kwa muda mrefu sekta yaSanaa imekuwa ikichukuliwa kama ya burudani tu kwa hiyo muda umefika wawatanzania kuichukulia Sanaa kama biashara na kuipa thamani halisi.

“Kwa sasa Sanaa imekubalika, ule wakati wa kuiona kama burudani tu umepita. Hatuna ujanjalazima tuirasimishe sekta ya Sanaa” alisisitiza.

 Aliwaahidi Wasanii kupitiamashirikisho na vyama vyao kuwa, kutakuwa na vikao vya mara kwa mara na kampunihii ili kuona ni kwa kiwango gani suala la udhibiti na utambuzi wa kazi zaokupitia nembo hii linaweza kutekelezwa.

1 comment:

  1. DIDA KILA SIKU UNASAFIRI KWA NINI HUNUNUI CAMERA YENYE UWEZO WA KUPIGA PICHA NZURI. PICHA UNAZOPOSTI KILA SIKU ZINATOKA VIBAYA KAMA WATU UNAWAANGALIA KWENYE MAJI. NAOMBA LIFANYIE KAZI HILI.

    ReplyDelete