PUMZIKA KWA AMANI RACHEL MWILIGWA

Tuesday, May 15, 2012 0 Comments

R.I.P RACHEL

MHARIRI wa Michezo wa gazeti la Mtanzania Rachel Mwiligwa jana alizikwa nyumbani kwao katika makaburi ya Tegeta A, Goba.

Mamia ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali, wadau wa michezo, sanaa pamoja na wabunge jana walijumuika na familia ya Rachel katika maziko hayo.Miongoni mwa wabunge waliohudhuria shughuli ya mazishi kuanzia kuaga mwili wa marehemu kwenye Kanisa la Anglikana Ubungo ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azan na Mbunge wa Ubungo John Mnyika.

Akimuelezea marehemu kanisani hapo, Mhariri wa Habari wa Mtanzania Kulwa Karedia alisema Rachel alikuwa mchapakazi na kwamba pengo lake halitazibika.

Mkurugenzi wa Redio Times Fm R.Nyaulawa akiteta jambo na Mbunge wa Ubungo John Mnyika


“Ni vigumu kuziba pengo la Rachel alikuwa mchapakazi hodari na nakumbuka alipanga kuanzisha gazeti lake, aliniambia alijipa miaka miwili tu katika kampuni yetu (New Habari 2006),”alisema.

Naye Katibu Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (Taswa) ambayo Rachel alikuwa mwanachama, George John akimzungumzia marehemu alisema alikuwa mstari wa mbele kukipigania chama.

Baadhi ya waombolezaji wakiupumzisha mwili wa marehemu Rechal Mwiligwa ktk nyumba yake ya milele kwao Goba jiini Dar es Salaam jana.
“Rachel mpaka mauti yanamkuta alikuwa mwanachama hai wa chama chetu, alikuwa akishirikiana kwa karibu na uongozi wa Taswa kutoa ushauri katika kukiendeleza chama”.

“Rachel atakumbukwa kwa kujiamini na kusimamia hoja, alikuwa akitoa hoja ataisimamia na kuitetea hata kama yuko peke yake mpaka aone anafanikiwa,”alisema.

Rachel alifikwa na umauti usiku wa Ijumaa kwenye Hospitali ya Mwananyamala Dar es Salaam alipokuwa amelazwa tangu Jumatatu iliyopita.

Rachel amewahi kufanya kazi kwenye vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo Mwananchi na Taifa leo.

Source; Habari.com

0 comments: