Mtanange wa BSS unaanza jumamosi hii, mambo ya Second Chance....

Thursday, June 23, 2011 0 Comments


Bongo Star Seach (BSS) kwa mwaka huu imepewa jina la BSS Second Chance.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Bench Mark Production ambayo ndiyo waandaaji wa shindano hilo, Rita Poulsen, alisema wameamua kufanya hivyo katika kusherehekea miaka mitano tangu kuanzishwa kwa shindano hilo mwaka 2006.

“Safari hii, BSS itajulikama kama BSS Second Chance’ lengo ni kuwapa nafasi wale walioshindwa ‘kutoka kimuziki… hawatashiriki washindi, hapana walioshinda hili si shindano lao kwani tutakuwa kama tunawadhalilisha,”alisema.

Alisema shindano hilo litaanza rasmi Jumamosi ya keshokutwa kwenye kituo cha runinga cha ITV kuanzia saa tatu usiku.

“Tumeamua mashindano ya mwaka huu tuyafanye Jumamosi maana wengi walikuwa wanalalamika kuwa Jumapili hawana muda wa kuangalia kutokana na kujiandaa na kazi siku inayofuata ambayo ni Jumatatu na kwa wanafunzi kujiandaa na shule, kwa hiyo msimu huu wa BSS itakuwa ni Jumamosi,”alisema.

Alisema jumla ya washiriki watakaopigiwa kura ni 34 ili kupata washiriki 14 watakaoingia kwenye jumba la BSS Second Chance ambao nao watapigiwa kura na watazamaji kama ilivyo kwenye mashindano yaliyopita mpaka kumpata mshindi atakayejizolea kitita.

“Mshindi aliyepita alipata Sh milioni 30, fikiria wa mwaka huu atapata Sh ngapi, zitakuwa ni fedha nyingi sana kwa vijana wetu,” alisema.

Aliwataja baadhi ya washiriki katika shindano hilo ni Kala Jeremiah aliyewahi kushiriki BSS ya mwaka 2006, Alice Peter aliyeshiriki BSS ya mwaka 2010, Feizal Ismail aliyeshiriki BSS ya mwaka 2008, Beatrice William aliyeshiriki BSS ya mwaka 2009 na Bella Kombo aliyeshiriki BSS ya mwaka 2010.

Kuhusu majaji, Rita alisema watakuwa walewale wa siku zote ila msimu huu ataongezeka mtazamaji ambaye atakuwa akiamua kupitia simu: Naye Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambayo ndiyo wadhamini wa shindano hilo George Kavishe alisema wanajivunia kuwa wadhamini tena wa shindano hilo.

0 comments: