AHSANTE MUNGU,JANA NILIPATA AJALI MAENEO YA MAKUMBUSHO NIKITOKEA KWANGU KIJITONYAMA NIKIELEKEA NDANI YA JENGO LA GREEN ACCERS SALOON.

Tuesday, February 01, 2011 2 Comments

Niliruhusiwa na magari mengine kuingia mara nikakutana na gari iliyokuwa imetanua kwa haraka ya kukwepa foleni nikamvaaa.
Mimi sikuwa na makosa bali yeye ndiye mwenye makosa alikiona kimbembe.
Hao majibaba waliosimama mbele ya hiyo gari yao ya silver wakijadiliana wanitoe vipi wakati jini langu makata keshapanda hakuna wakunigusa.
Sungura kamkaba tembo namaanisha hii ndio gari iliyonigonga sababu ya udogo wake lkn imenifumua vya kutosha ni hayo yaliyonikuta jana waungwana namshukuru mungu sijaumia popote maisha yanaendelea ila kajifunza kutanua barabrani hakufai fuata njia kihalali sasa hivi mie mguu juu yeye kalipia matengenezo ilo nalo sakata.

2 comments:

  1. mamy pole ndio mambo ya barabarani tunashukuru kama ujaumia popote polesana mamito.





    Amina Zangira

    ReplyDelete
  2. vizuri hujaumia dear, tusubiri shigongo aandike na kwake

    ReplyDelete