MASHAUZI CLASSIC kupagawisha Buriaga, Temeke Ijumaa hii... Baikoko, Welawela kuonyesha nyonga za Ukweli!

Tuesday, November 29, 2011 1 Comments

Kundi zima la Mashauzi Classic Modern Taarab likiongozwa na Isha Mashauzi aka 'Jike la Simba' litafanya show kabambe ktk ukumbi wa BURIAGA maeneo ya Temeke Wailes jijini DSM Ijumaa hii ya tarehe 02 Dec. 2011.




Ktk show hio Mashauzi Classic wataimba nyimbo nyimbo zao zote pamoja na kutambulisha nyimbo mpya kwa wakazi wa Temeke. Sambamba na Kundi hilo la taarab kutakuwa na show kali kutoka kwa Baikoko na wanenguaji wake wakichuana na kikundi cha wanenguaji cha Welawela.



Welawela kazini



Wanenguaji wa Baikoko kutoka Tanga wakionyesha umahiri wa kuzungusha nyonga.



Weraweraaaaaaaaa mwanamke nyonga, makalio hata paka wako anayo!


Mbali na Burudani hio ya kukatwa na Shoka, pia MSAGA SUMU msanii huru wa kopi za taarab atakuwepo.

1 comment:

  1. picha nzuri lakin mpendwa tafta kamera nzuri picha zako zinagiza sana mamie ni mdau wako wa ukweli sijakukukosoa kwa ubaya waosha vinywa msinitafte ehhehe

    ReplyDelete