CHANGIA DAMU, KUOKOA MAISHA YA MTANZANIA MWENZAKO

Wednesday, November 30, 2011 0 Comments

https://mail.google.com/mail/?ui=2&ik=dacc13d1ce&view=att&th=133e23efd17df628&attid=0.1&disp=inline&zw

Kila mwaka Tanzania hupokea asilimia 30 ya damu zinazohitajika ktk hospitali zake. Utafanya nini kama wewe mwenyewe au mtu unayemjua akiwa anahitaji damu kwa dharura? Klabu ya Rotaract ya Dar es Salaam inaratibu ukusanyaji wa damu katika maeneo kadhaa jijini Dar es Salaam, ijumaa Desemba 2 na 3 kuanzia saa 02:00-12:00 jioni.

Tafadhali angalia Kipeperushi hapo juu kwa maelekezo ya maeneo ya vituo vya kuchangia damu ijumaa na jumamosi.

Lengo ni kukusanya vipande 1,500 vya damu ya kusaidia watoto katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Damu ya ziada itakayokusanywa itatumika kwa wale wanaohitaji matibabu ya dharura katika hospitali ya jirani.

Ukusanyaji damu utafanyika kufuatia uzoefu wa kimataifa ktk viwango bora kwa wakusanyaji kuthibitishwa
kutokea National Blood Transfusion Services na hospitali ya Muhimbili -Usafi , Usalama.

Toa damu ukielekea Mwaka Mpya huku ukijua ya kuwa binafsi umesaidia kuokoa maisha.

0 comments: