NANDO......MH! NJE YA BIG BROTHER THE CHASE

Monday, July 29, 2013 4 Comments

Mshiriki wa kiume toka Tanzania aliyekua anatuwakilisha katika shindano la Big Brother Africa "The Chase" leo ametolewa nje ya jumba hilo na kusitisha uwepo wake katika shindano hilo lililojipatia umaarufu sana barani Afrika.
Breaking News: Nando Disqualified-Elikem gets a Strike


Tukio hilo limetokea baada ya kua zoezi la EVICTION limepita na washiriki wawili ANABEL (Kenya) na SULU (Zambia) kua ndio waliopata kura chache baada ya kua nominated na kutoka.
Big brother au BIGGIE aliwakusanya House-mates wote Living room na kuwawekea clip ya malumbano kati ya NANDO na ELIKEM yaliyotokea Ijumaa ambapo walitukanana sana, lakini chanzo cha ugomvi huo kikionekana kua ni Nando.


Mbali na ugomvi huo NANDO aliwahi kukamatwa na KISU katika party ya Channel O jumamosi moja akapewa onyo. Ugomvi wa Ijumaa lilikuwa kosa la 2 na kosa la 3 aliloambiwa kwenye diary room ni kuongea maneno ya vitisho dhidi ya ELIKEM kua..."I feel like stabbing him. A nigga like that deserves to die".Pamoja na kukamatwa na Mkasi chini ya kitanda chake, basi bwana NANDO safari yake ikawa imeishia hapo.



Kwa walio tazama inasikitisha sababu hakupata hata nafasi ya kuagana na wenzake. 

Kwa nchi yetu hili ni tukio la pili sasa kwa mshiriki kua disqualified, kama utakumbuka katika BBA Amplified, LOTUS alitolewa kwa kumchapa mshiriki mwenzie kibao (Kofi).  

POLE KWETU WATANZANIA, POLE KWA NANDO..... Mungu amsaidie FEZA KESSY aje na mkwanja.

4 comments:

  1. FEZA ATATOLEWA TU HIVI KARIBUNI MAANA SHUGHULI ILIYOMPELEKA KULE AMEIACHA, KUCHA KUTWA KUKUMBATIANA NA HICHO KIDUME, WALA HACHEZI GAME TENA. I'M SPEECHLESS. HALAFU JANA KASHINDWA HATA KUMSAIDIA BIMPY KU-PACK MIZIGO YA NANDO. YAANI !!!

    ReplyDelete
  2. sawasawa Feza alivyoacha kutoa ushilikiano wa ku-pack mizigo ya huyo chizi,yaani Nando kaniboa mimi,vibaya mnooo,Sifa ,dharau,majigambo,kama shida zako ni huko home,sio kwenye Game Lol..

    ReplyDelete
  3. Watu wengi wanasema FeZa out so nadhani next week FeZa naye tz.

    ReplyDelete
  4. I AM PROUD OF NANDO FOR ONLY NOT TO APPOLOGIZE TO ELIKEM!!
    HEY HE LEFT WITH HIS PRIDE!!!!

    ILA MAKOSA MENGINE NAMI NIMEUMIA SANA COZ ALIKUWA AKIWAKILISHA VIZURI.

    NANDO YUKO STRAIGHT NA HAOGOPI KUSEMA CHA MOYONI NDIYO MAANA WATU WANAMCHUKIA. I LOVE PPL LIKE HIM.

    FOR ME NANDO U'RE THE BEST, COZ HATA KAMA UNGEOMBA SAMAHANI NDANI YA HIZO 24HRS STILL ELIKEM ANGEKU-SWAPP

    ReplyDelete