Mshindi wa BSS mwaka huu kujinyakulia Shs. millioni 50, amezungumza makamu
wa Rais wa Kampuni ya Zantel, Ahmed Mokhles kuhusiana na kampuni yao kudhamini shindano
la kusaka vipaji la Bongo Star Search.
|
Master J |
|
Shaa |
|
Mkurugenzi wa Benchmark Production Madam Rita, waandaaji wa BSS |
|
Wasanii na wadau waliohudhuria ktk uzinduzi wa BSS Serena Hotel Dsm |
Shindano la BSS mwaka huu litajulikana kama ‘Epiq Bongo Star Search’ ambapo mshindi atanyakua shilingi
milioni 50 tofauti na millioni 40 ya mwaka jana pamoja na zawadi nyingine kutoka Zantel, sambamba na
mkataba wa kurekodi ili aweze kuendeleza kipaji chake baada ya shindano
hilo.
Mchakato wa mwaka
huu utawahusisha washiriki kutoka mikoa nane tofauti na saba ya mwaka jana Zanzibar,
Lindi, Mbeya, Mwanza, Arusha, Tanga, Dodoma na Dar es Salaam
mchakato utaanza mwezi Juni na pia wamepunguza umri wa kushiriki kutoka miaka 18 mpaka 16 sasa.
0 comments: