FLAVIANA MATATA ATOA MSAADA WA MABOYA 500 YA KUJIOKOLEA MAJINI, KATIKA KUMBUKUMBU YA AJALI YA MV. BUKOBA MIAKA 16 ILIYOPITA

Tuesday, May 22, 2012 0 Comments

Flaviana Matata akikabidhi msaada wa maboya 500 kwa mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Elias Makori kulia ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 16 ya ajali ya meli ya MV Bukoba, anayeshuhudia ni Meneja Masoko na Biashara wa Shirika la usafirishaji wa majini mkoani Mwanza la Marine Service,Kapten Obadia Nkongoki.
 Mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya kuokolea maisha ya watu katika vyombo vya usafiri wa maji ambavyo vimelengwa maalum kwa Ziwa Viktoria mjini Mwanza. Msaada wa vifaa hivyo umeelekezwa katika shirika la kiserikali la usafiri wa maji jijini Mwanza lijulikanalo kama Marine Service Co. Ltd.
Flaviana Matata ametoa jumla ya vifaa hivyo 500 (vyombo vya kuokolea maisha ndani ya maji) ikiwa ni kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya Mv.Bukoba mnamo May 21 mwaka 1996 ambapo pia alimpoteza mama yake
mzazi katika ajali hiyo iliyouwa watu takribani 1,000. Sababu mojawapo kubwa iliyofanya watu kupoteza maisha yao siku ya tukio hilo ilikuwa upungufu na ukosefu wa vifaa vya majini kama maboya (Live Vest).
‘Naamini kwamba, watu waliofariki katika ajali ya meli ya Mv Bukoba wengi walipoteza uhai wao kwa sababu walikosa vifaa vya kujikwamua ndani ya maji, hivyo ndo maana nimeamua leo katika kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba nije kutoa msaada wa vifaa hivi 500’ alieleza Flaviana Matata.
Vilevile akaongeza kuwa ni vyema vyombo vya majini vikawa na utaratibu
wa kutoa elimu na maelekezo jinsi ya kutumia maboya endapo kutatokea
tatizo kabla ya kuanza kwa safari kama wafanyavyo katika usafiri wa anga.

0 comments: