WAPENZI WA SOKA KUMUAGA MAREHEMU MAFISANGO LEADERS KESHO ASUBUHI
MWILI wa aliyekuwa kiungo mkabaji wa
Simba ya Jijini Dar es Salaam, Patrick Mutesa Mafisango, aliyefariki
dunia usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya gari maeneo ya Tazara, Dar es
Salaam unatarajiwa kuagwa kesho saa 2 asubuhi katika viwanja vya Leaders
Club, Kinondoni.
Meneja wa Simba SC, Nicodemus Nyagawa amesema kuwa, baada ya zoezi la
kuagwa mwili huo, utasafirishwa kwa ndege ya Shirika la ndege ya
Kenya,KQ kuelekea nchini Kigali Rwanda kwa shughuli za mazishi.
Wapenzi
wa Simba na Mashabiki wa Soka wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuaga
mwili wa marehemu Mafisango, aliyekuwa kiungo tegemeo wa klabu hiyo
katika msimu wake mmoja wa kuichezea tangu ajiunge akitokea Azam FC.
Akielezea
chanzo cha ajali hiyo, Nyagawa alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa
alizopata ni kwamba, Mafisango aliyekuwa akiendesha gari lake mwenyewe,
alikuwa akijaribu kumkwepa dereva wa pikipiki na kwa bahati
mbaya akaingia mtaroni na kuumia kabla ya kufariki dunia.
0 comments: