R.I.P PATRICK MAFISANGO
Mchezaji mahiri wa Klabu ya Wekundu wa msimbazi Simba na timu ya Taifa ya Rwanda PATRICK MAFISANGO amefariki alfajiri ya leo baada ya kupata ajali ya gari.
Wakiwa ktk shamrashamra za kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara wachezaji wa Simba akiwamo marehemu walitarajia kuzuru ktk studio za 100.5 Times Fm leo mchana kwa ajili ya Interview kuhusiana na Sherehe waliyoiandaa kufanyika pale Traverntine Magomeni kesho kutwa
Taarifa hizi za kusikitisha zinaendelea kutolewa tutajuzana taratibu zingine zinazofuata
Enzi za uhai wake, Mafisango akiwa amebebwa juu juu akishangiliwa na wadau
Gari aliyopata nayo ajali usiku wa kuamkia leo
Blogu ya Mitikisiko inatoa pole sana kwa familia, ndugu jamaa na marafiki, wana-Simba, wanasoka wote ulimwenguni
MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
0 comments: