Isha Mashauzi kumsindikiza Mkubwa Fella katika mpambano wa Nani mkali katika wasanii Kizazi kipya cha Taarab, tarehe 1 July. Equator Grill Temeke!.
Mkubwa FELLA kiongozi wa kundi la bongo fleva TMK Family yakina Temba na Chegge, ambaye pia ni msanii chipukizi ktk Taarabu atachuana na wasanii wengine watatu chipukizi ktk miondoko hio ya muziki wa Taarabu ktk kumtafuta Mkali nani kati yao Ijumaa hii pale EQUATOR GRILL, Mtoni kwa Aziz Ally
Show hio ya aina yake itaanza mishale ya saa 2 usiku huku ikiongozwa na Kings Modern Taarab wanaotamba na nyimbo kibao kwasasa ikiwemo "Kijoka" na kusindikizwa na ISHA MASHAUZI mkali wa "Mama nipe Radhi" na zingine nyingi.
Wasanii wa kizazi kipya cha Taarab watakaopanda jukwaani kuoneshana nani mkali ni wale wanaotamba sana ktk medani hizo ambao ni Mkubwa Said Fella na nyimbo yake ya "Simuachi"aliyomshirikisha Isha, Athumani Ally "Nyongo mkalia ini", Omary Ally "Simuachi mpenzi wangu" na Kepteni Temba "Nimeiteka himaya".
Akimalizia kunihabarisha mratibu wa onyesho hilo la mpambano alisema kiingilio kitakuwa ni Tshs. 5000/= na wapenzi na mashabiki wote wa burudani kutoa maamuzi NANI MKALI KATI YAO!!!!!!
Dida, tafadhali naomba ubadili theme/background ya blog yako. Unajua nini.. nimechunguza nikagundua hii background iko kama imetingishika hivi yaani haiko clear. Basi inafanya hata picha unazotoa, rangi ya picha na vitu vingine kuwa na huo mtingishiko fulani. yaani haina mngaro unaovutia. Hebu consider hilo jaribu kubadilisha theme/backround ujaribu kuweka kama za blogers wengine.. mfano kama dina marious haina background picture yoyote, au ya lady jay dee,.. try it na utaona matokeo yake. Hivi ilivyo inakuwa blog kama imepooza fulani hivi machoni kwa watazamaji. Sijui wadau wengine mnaonaje ila mimi hayo ni maoni yangu.
ReplyDelete