FFU wa Ngoma Africa band jukwaani Heidelberg City, Ujerumani..

Wednesday, June 15, 2011 1 Comments


Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" almaarufu FFU,

imejikuta katika mshike mshike usio na mwisho uko nchini ujerumani..kwani bendi hiyo

inaparamia jukwaa la AFRIKA DAYS Festival siku ya jumamosi 25.06.2011 kuanzia saa 3 usiku katika mji wa Heidelberg,Ujerumani, ambako washabiki wa miji ya Heidelberg,Mennheim,n.k watajirusha na gwaride la mziki wa FFU ndani ya ukumbi Karlstorbahnhof,mjini Heidelberg.


Jumapili ya 26.06.2011 Kikosi kazi Ngoma Africa band aka FFU watatumbuiza katika onyesho lingine kubwa la "Afrika Tage" litakalofanyika mjini Freudenstadt,kusini mwa Ujerumani,ambako nako kutakuwa na pata shika nguo kuchanika kati ya washabiki na "Bongo Dansi".

FFU pia wameongeza Dozi la nguvu katika kambi yao www.ngoma-afrika.com ambako nyimbo za "Rushwa ni adui wa haki" na lile sebene la "Amiri Jeshi Mkuu" zinaweza kusikika. Zogo la "Baba wa kambo" bado linaendelea at www.ngoma-africa.com


raha jipe mwenyewe

1 comment:

  1. hallo dida sijajua kumbe hili blog lako sio siri nikilifungua naskia kichefuchefu kama vipi please close down sio siri hili blog limekaa kama mavi hata halisisimui,udaku na ushambega,halivutii hata kidogo sorry for my comments ila ukweli ndo huo,kwa maelezo zaidi wasiliana na mimi thru my number,0712774560.ciao

    ReplyDelete